TUME YA MADINI

CONTACT US | FAQs | STAFF MAIL | ENGLISH / SWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF MINERALS

 THE MINING COMMISSION

madini

MINING COMMISSION SHOWCASED OPPORTUNITIES AT 2024 MINING CONFERENCE

Dar es Salaam, 19th November 2024 The Mining Commission actively participated in the Tanzania Mining and Investment Conference 2024, held at the Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) in Dar es Salaam. Conducted under the theme “Mineral Value Addition for Social-Economic Development,” the event brought together key stakeholders, government officials, and investors from across the globe to explore opportunities in Tanzania’s mining sector. During the opening ceremony, Prime Minister Kassim Majaliwa reaffirmed the government’s commitment to promoting mineral value addition, emphasizing its role in fostering industrialization and accelerating economic growth. Addressing participants, Minister for Minerals Hon. Anthony Mavunde detailed the achievements of Tanzania’s mineral sector and highlighted government-led initiatives designed to support small-scale miners. He encouraged both local and international investors to seize opportunities in mining, mineral processing, and trade, emphasizing Tanzania’s readiness to collaborate on advancing the industry. The Mining Commission showcased its efforts to enhance mineral processing and value addition through interactive engagements with stakeholders and potential investors. Visitors to the Commission’s booth were informed about the country’s progressive policies and investment incentives, which aim to position the mining sector as a cornerstone of the national economy. The conference served as a testament to Tanzania’s dedication to leveraging its mineral resources as a driver of sustainable development, job creation, and technological advancement.

MINING COMMISSION SHOWCASED OPPORTUNITIES AT 2024 MINING CONFERENCE Read More »

WAZIRI MAVUNDE AELEKEZA KUFUTWA KWA LESENI NA MAOMBI YA LESENI 2648

Jumla ya eneo la ekari Milioni 13 zinashikiliwa na watu 6 Awataka wenye Leseni za utafiti kutowatumia wachimbaji wadogo kama sehemu ya utafiti Maeneo mengi kugawiwa vikundi vya wachimbaji wadogo na wawekezaji wenye uwezo wa kuchimba Wamiliki wa Leseni wadaiwa Bilioni 36 kwa kushindwa kulipa Zoezi hili kuwa endelevu kuondoa ubabaishaji katika sekta ya madini Dodoma Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amemuelekeza Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, kufuta jumla ya maombi na Leseni za Utafiti 2648 ili kupisha waombaji wengine kupata fursa ya kuomba na kuendeleza maeneo hayo kwa manufaa ya Taifa na ukuzaji wa Sekta ya Madini. Waziri Mavunde amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya wamiliki wa leseni ambao wamekuwa hawazingatii utekelezaji wa majukumu yao ya umiliki wa leseni kwa Mujibu wa Sheria ya Madini, Sura 123. Miongoni mwa makosa ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ni pamoja na wamiliki wengi wa leseni kutoanza au kutoendeleza maeneo ya leseni zao na badala yake kuhodhi maeneo; kutolipa ada stahiki za leseni; kutowasilisha nyaraka muhimu kama Mpango wa Ushirikishwaji wa Watanzania Kwenye Shughuli za Madini (Local Content Plan), Mpango wa Wajibu wa Makampuni kwa Jamii (Corporate Social Responsibility) na nyaraka za taarifa za fedha kuonesha matumizi yaliyofanyika pamoja na vielelezo vya matumizi husika. “Ninatoa mfano kuna watu 6 tu wanahodhi maeneo yenye ukubwa wa ekari milioni 13 ukubwa wa maeneo hayo ni sawa na ukubwa mara nne wa Mkoa wa Kilimanjaro na hayafanyiwi chochote ili hali mahitaji ya maeneo ya uchimbaji ni mkubwa sana hapa nchini na hasa kwa wachimbaji wadogo ambao wamekuwa na mchango mkubwa sana kwenye kukuza sekta ya madini. Kuna watu wenye Leseni za utafiti ambao hawatimizi masharti ya Leseni zao na hivyo kutegea uwepo wa wachimbaji wadogo kama mgongo wa utafiti wao,” amesema Mavunde. Kutokana na kosa la kutolipa ada stahiki za leseni, kiasi cha takribani Shilingi bilioni 36 zinadaiwa kutoka kwa wamiliki na waliokuwa wamiliki wa Leseni za Utafutaji wa Madini, Leseni za Uchimbaji Mdogo wa Madini na Leseni za Uchimbaji wa Kati na Mkubwa wa Madini. Kufuatia uwepo wa makosa hayo, Tume ya Madini imetoa Hati za Makosa kwa jumla ya leseni 59 hai kwa sababu wamiliki wake hawajatekeleza masharti na matakwa mbalimbali ya umiliki wa leseni husika. Mbali na wamiliki wa leseni, kumekuwa na baadhi ya waombaji wa leseni ambao wamekuwa wakitumia fursa ya uwepo wa teknolojia rahisi ya uwasilishaji wa maombi ya leseni – yaani mfumo wa Online Mining Cadastre Portal vibaya kwa kuwasilisha maombi mengi bila ya kulipa ada stahiki na wengine kuwasilisha maombi bila ya kuambatisha nyaraka zinazotakiwa kuwasilishwa pamoja na maombi ya leseni. Katika uchambuzi uliofanywa na Tume ya Madini, imebainika kuwa, hadi Februari, 2024 kuna jumla ya maombi 2,180 ambayo hayajalipiwa ada stahiki za maombi. Vilevile, katika uchambuzi uliofanya na Tume ya Madini imebainika kuwa, hadi Februari, 2024 kuna uwepo wa maombi 409 ya muda mrefu ambayo wamiliki wake wamelipa ada za maombi lakini hawajawasilisha nyaraka muhimu zinazoambatana na maombi hayo.

WAZIRI MAVUNDE AELEKEZA KUFUTWA KWA LESENI NA MAOMBI YA LESENI 2648 Read More »

TANZANIA YAANDIKA HISTORIA KUWA NA MGODI WA MADINI TEMBO, KIWANDA CHA KISASA CHA USAFISHAJI METALI

-Eneo la Tajiri- Handeni lina tani milioni 268 za mashapo ya Madini Tembo ikijumuisha tani milioni 74 za mashapo yaliyothibitika -Mgodi kuingizia Serikali Mapato dola za Marekani milioni 437.96 (Trilioni 1.12 Tshs) kutokana na gawio la hisa za Serikali, kodi na tozo -Kiwanda kuchakata na kuzalisha metali zenye ubora Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa Tanzania imeandika historia kwa kuwa na mgodi mkubwa wa uzalishaji wa Madini Tembo na kiwanda kikubwa cha Usafishaji wa Madini ya Metali-Anuai, Miradi itakayochochea Ukuaji na Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa na maendeleo ya kiuchumi nchini. Aliyasema hayo Machi 21, 2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Leseni ya Uchimbaji Mkubwa Madini Tembo (Heavy Mineral Sands) kwa Kampuni ya Nyati Mineral Sands Limited na leseni ya Kiwanda cha Uchenjuaji wa Madini ya Metali kwa Kampuni ya Tembo Nickel Refining Company Limited. Akizungumzia Mradi wa Uchimbaji Mkubwa wa Madini Tembo, Waziri Mavunde alisema kuwa, katika shughuli ya Utafiti wa Madini iliyofanywa na kampuni tanzu ya Jacana Resources ilibaini kuwa eneo la Tajiri lilopo Wilaya ya Handeni mkoani Tanga lina kiasi cha takribani tani milioni 268 za mashapo ya madini ya heavy mineral sand ikijumuisha tani milioni 74 za mashapo yaliyothibitika. Kuhusu Kiwanda cha kuchakata Madini ya Metali-Anuai cha Tembo Nickel Refining Limited kitakachojengwa Kahama mkoani Shinyanga, Mhe. Mavunde alisema kuwa, ujenzi wake utakuwa ni utatuzi wa changamoto iliyokuwepo kwa Wachimbaji wa Madini ya metali nchini kulazimika kusafirisha makinikia ya metali kwenda kwenye viwanda vya nje ya nchi kwa ajili ya uchenjuaji ili kupata zao la mwisho au kuuza madini katika hali ya makinikia kwa bei ya chini. “Kwa kupitia teknolojia hiyo makinikia yatakayozalishwa katika mgodi wa Kabanga na mingine nchini yataweza kuchakatwa na kuzalisha metali zenye ubora.” alisisitiza Mavunde. Vilevile, Mhe. Mavunde alitoa wito kwa Wachimbaji na Wamiliki wa Migodi inayozalisha makinikia nchini kutumia kiwanda hicho kuchakata madini hayo pindi kitakapo kamilika ili kukuza fursa za ajira na mapato yatokanayo na rasilimali madini. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nyati Mineral Sands Limited, Jozsef Patarica alisema kwamba Mradi huo utaleta manufaa makubwa kwa Tanzania kwani utasaidia kuongeza maarifa, kutengeneza ajira lakini pia kuchangia mapato ya Serikali kupitia kodi mbalimbali. Kampuni ya Nyati Mineral Sands Limited ni Kampuni ya ubia baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye umiliki wa hisa asilimia 16 na Kampuni ya Strandline Resources Limited ya Australia yenye umiliki wa asilimia 84 ambapo Serikali inatarajiwa kukusanya mapato takribani dola za Marekani milioni 437.96 (Trilioni 1.12 Tshs) kutokana na gawio la hisa za Serikali, kodi na tozo mbalimbali; kupatikana kwa fursa za ajira za moja kwa moja zipatazo 150 ikijumuisha ajira 140 za watanzania na 10 za wageni. Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Lifezone Metals kwa niaba ya Kampuni ya Tembo Nickel, Chris Showalter alisema kuwa Kiwanda hicho cha Uchenjuaji cha Kahama ni kielelezo cha mafanikio ya Tanzania na kwamba hatua hiyo ni kuandaa jukwaa pana litakalobeba kitovu cha uchimbaji, uchakataji na uchenjuaji wa madini ndani ya Ukanda Maalum wa Kiuchumi wa Buzwagi wilayani Kahama mkoani Shinyanga “Tutachimba, tutachakata, tutachenjua Madini ya Kimkakati hapa hapa nchini” alisisitiza Showalter. Kiwanda cha Usafishaji wa Madini kitamilikiwa na Kampuni ya Tembo Nickel Refining Limited ambayo ni Kampuni tanzu ya kampuni ya ubia ya Tembo Nickel Corporation Limited ambayo inamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya Lifezone Metals ya Uingereza iliyosajiliwa katika soko la hisa la Marekani (NYSE:LZM). Matukio hayo mawili yalikwenda sambamba na tukio la uhuishaji wa Leseni ya Uchimbaji Madini ya Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu uliopo Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick Gold Mine.

TANZANIA YAANDIKA HISTORIA KUWA NA MGODI WA MADINI TEMBO, KIWANDA CHA KISASA CHA USAFISHAJI METALI Read More »

HAFLA YA KUKABIDHI LESENI

“Mheshimiwa Waziri, Mkoa wa Tanga una kiasi kikubwa cha Madini Tembo kuliko mkoa wowote hapa nchini, na tunapata leseni kubwa ya Uchimbaji Madini haya ni imani yetu kwamba pindi Mradi huu utakapoanza shughuli shughuli za uzalishaji katika eneo la Tajiri wilayani Pangani itafungua fursa nyingi za ajira, biashara kwa Wananchi wetu pamoja na Uchumi na Maendeleo ya Mkoa wetu wa Tanga.” Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Batilda Buriani

HAFLA YA KUKABIDHI LESENI Read More »

” THE MINING COMMISSION’S ROLE IN TRANSFORMING THE MINING SECTOR”

Three years of President Samia………. 42 mineral markets and 99 buying centers have been established. The speed of issuing mining licenses has increased from 5,094 in 2018/19 to 9,642 in 2022/23. Collections have tripled from 213.3 billion shillings in 2016/17 to 677.7 billion shillings in 2022/23. “Minister Mavunde Earns High Praise from Small-Scale Miners for Sector Support” To ensure the Mining Sector significantly contributes to the country’s economic growth, the Government has made various efforts, including amending the Mining Law of 2010. The Mining Commission was established under the Mining Act 2010, as amended by the Written Laws (Miscellaneous Amendment) Act 2017. The Commission came into existence through Government Notice No. 27 issued on July 7th, 2017. It has assumed all operational functions previously performed by the Minerals Division under the Ministry of Energy and Minerals, as well as those carried out by the Tanzania Minerals Audit Agency (TMAA) and Tanzania Diamond Sorting Organization (TANSORT). Explaining the responsibilities of the Mining Commission briefly, Eng. Yahya Samamba, the Executive Secretary of the Commission, explains that they include issuing and managing mining licenses, overseeing exploration and mining activities, as well as conducting inspections of mines and the environment. Additionally, while commending the efforts made by the President of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Samia Suluhu Hassan, Engineer Samamba highlights that since the establishment of the Mining Commission, many citizens have observed significant changes in the Mining Sector and have gained increased confidence in both the President and the Government as a whole. Explaining the status of revenue collection before and after the establishment of the Commission, Eng. Samamba elucidates that revenue collection increased from 213.3 billion shillings during the financial year 2016/17 to 677.7 billion shillings during the financial year 2022/2023. “During the financial year 2022/2023, as the Mining Commission, we were given the target of collecting 822 billion shillings and succeeded in collecting 677.7 billion shillings, achieving 82.45%. In the period of the financial year 2023/2024, we have been tasked with collecting 882 billion shillings, a target I firmly believe we will surpass,” emphasizes Eng. Samamba. Eng. Samamba attributes the secret of success in revenue collection to the patriotism and creativity of the employees at the Mining Commission Headquarters, Resident Mines Offices, and Mines Resident Offices, as well as the excellent cooperation from the leaders of the Ministry of Minerals. Furthermore, discussing the mineral markets established in the country, Eng. Samamba explains that they were set up as a means to assist small-scale miners in finding a reliable market for their minerals post-mining, enabling the Government to generate income and obtain accurate statistics on minerals produced by small-scale miners. The aim is to sell minerals according to the indicative prices provided by the Mining Commission, based on global market trends and to control the smuggling of minerals by unscrupulous miners and traders. He adds that up to now, the Mining Commission has established 42 mineral markets and 99 buying centers across the country, which have increased the contribution of small-scale miners to revenue collection from five (5) percent to forty (40) percent in 2022/2023. He emphasizes that mineral markets have significantly reduced the speed of mineral smuggling and have introduced competition among mineral dealers through these markets and buying centers. Explaining the Government’s strategies in controlling mineral smuggling and ensuring the increasing value of tanzanite, Eng. Samamba states that in 2018, the Government decided to construct the Mirerani wall in Simanjiro District, Manyara Region, which has significantly benefited both the miners and the Government. He further explains that other strategies set by the Government include relocating mineral dealers from Arusha to Mirerani, with the aim of boosting the economy of the Mirerani area and curbing mineral smuggling. In another aspect, explaining how the government addresses the issue of Tanzanian participation in the mining sector, he states that in recognition of its importance, in 2018, the government established various rules and guidelines to ensure Tanzanian involvement in exploration and mining activities. This involvement includes providing various services in mines such as transportation, agricultural products, security, insurance, law, banking, etc. He states that until the year 2022, 86 percent of goods and services are provided by Tanzanian companies to large mining companies, while 14 percent are provided by foreign companies through a special permit issued by the Mining Commission. Regarding employment in the mines, 96 percent are Tanzanians, while foreign nationals make up four (4) percent. “It should be understood that no company is allowed to import goods or services from abroad without obtaining permission from the Mining Commission. Our goal is to ensure that every Tanzanian benefits from the Mining Sector,” emphasizes Eng. Samamba. In another aspect, the Mining Commission has been carefully managing to ensure that mining companies provide services to the surrounding community (CSR) as directed by the Mining Law. Eng. Samamba emphasizes that the issue of safety in mines cannot be overlooked for the success of the Mining Sector. Recognizing this, the Mining Commission, through the Mines Inspectorate and Environment Department, has been conducting regular inspections in mines as well as providing education. He continues by mentioning other achievements, including the increase in the issuance of mining licenses from 5094 licenses in the financial year 2018/2019 to 9642 licenses in the financial year 2022/2023. He adds that the contribution of the Mining Sector to the National GDP increased from 4.4 percent in 2017 to 9.1 percent in 2022. Eng. Samamba concludes by stating that many foreign companies have continued to show interest in investing in the Mining Sector due to the great work done by the President of the United Republic of Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan, in advertising the opportunities available in the country. Speaking on behalf of small-scale miners in Tanzania, Kulwa Mkalimoto, the Chairman of the Dodoma Regional Miners Association (DOREMA), extended congratulations to the Minister for Minerals, Hon. Anthony Mavunde, for his support of small-scale miners and for addressing the challenges they have encountered in the mineral sector. “The Minister of Minerals

” THE MINING COMMISSION’S ROLE IN TRANSFORMING THE MINING SECTOR” Read More »

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA TUME YA MADINI MAKAO MAKUU JIJINI DODOMA

Ujenzi wake wafikia asilimia 87.5 Yamtaka Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi Dodoma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, leo Machi 19, 2024 ikiongozwa na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali imefanya ziara kwenye mradi wa ujenzi wa Jengo la Tume ya Madini Makao Makuu jijijni Dodoma kwa ajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wake. Viongozi wengine waliokuwepo ni pamoja na Watendaji kutoka Wizara ya Madini, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Wakurugenzi na Mameneja kutoka Tume ya Madini. Mara baada ya kufanya ziara na kupata maelezo kutoka kwa mkandarasi, imemtaka mkandarasi kuhakikisha anakamilisha kazi kwa kiwango bora na kwa wakati ili watumishi wa Tume ya Madini waanze kutumia jengo hilo mara moja. Wakati huo huo akizungumza kwenye eneo la mradi, Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa amesema kuwa Wizara ya Madini itahakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu. Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali sambamba na kupongeza Kamati kwa kutembelea mradi ameongeza kuwa Wizara ya Madini itasimamia ujenzi wa mradi kwa karibu zaidi kwa kila hatua ili kuhakikisha mradi unakamilika ifikapo Aprili 24, 2024. Awali akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Jengo, Katibu Mtendaji wa Tume, Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa hadi sasa ujenzi wa jengo umefikia asilimia 87.5 na kuongeza kuwa sehemu iliyobakia ya asilimia 12.5 inakusudiwa kukamilishwa ndani ya kipindi kilichobaki. Mhandisi Samamba amesema kuwa mradi huu utakapokamilika utawezesha watumishi wote wa Tume ya Madini Makao Makuu kuwa katika jengo moja hivyo kuimarisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi na wadau wengine.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA TUME YA MADINI MAKAO MAKUU JIJINI DODOMA Read More »

“SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA MAZURI KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI” – MHANDISI SAMAMBA

Dodoma Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa Serikali kupitia Tume ya Madini itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini kama mkakati wa kuhakikisha mchango wao kwenye Sekta ya Madini unaendelea kukua sambamba na kuzalisha ajira zaidi. Mhandisi Samamba ameyasema hayo leo Machi 18, 2024 kwenye kikao cha sita cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Madini kilichofanyika jijini Dodoma ambacho kimeshirikisha Wakurugenzi, Mameneja, Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa, watumishi na wageni waalikwa kutoka TUGHE, na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Amesema kuwa, mchango wa wachimbaji wadogo kwenye mapato yatokanayo na Sekta ya Madini umeendelea kukua kutoka asilimia tano (5) hadi asilimia arobaini (40) Mwaka 2022/2023 na kusisitiza kuwa Tume ya Madini itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa wachimbaji wadogo sambamba na kutatua changamoto mbalimbali. Akielezea mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa Tume ya Madini, Mhandisi Samamba amesema kuwa ni pamoja na ongezeko la ukusanyaji wa maduhuli kutoka shilingi bilioni 213.3 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 hadi shilingi bilioni 677.7 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023. “Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 kama Tume ya Madini tulipewa lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 822 na kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 677.7 ikiwa ni (82.45%) na katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 tumepewa lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 882 ambalo ninaamini kabisa tutalivuka,” amesema Mhandisi Samamba. Mhandisi Samamba ameendelea kusema kuwa siri ya mafaniko kwenye ukusanyaji wa maduhuli ni pamoja na uzalendo na ubunifu wa watumishi wa Tume ya Madini Makao Makuu, Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa, Maafisa Migodi Wakazi na ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Madini. Ameendelea kueleza mafanikio mengine kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko ya madini 42 na vituo vya ununuzi wa madini 100 nchini, ongezeko la utoaji wa leseni za madini kutoka leseni 5094 katika mwaka wa fedha 2018/2019 hadi leseni 9642 katika mwaka wa fedha 2022/2023, kudhibiti utoroshaji wa madini na kupungua kwa ajali kwenye migodi ya madini kutokana na kaguzi zinazofanywa mara kwa mara kwenye shughuli za uchimbaji wa madini sambamba na kutolewa kwa elimu. Amefafanua mafanikio mengine kuwa ni pamoja na ongezeko la ushiriki wa kampuni za kitanzania kwenye utoaji wa huduma kwenye migodi kutokana na maboresho ya kanuni za ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini ambapo hadi kufikia mwaka 2022 asilimia 86 ya bidhaa na huduma zinatolewa na kampuni za kitanzania kwenye kampuni kubwa za uchimbaji wa madini huku asilimia 14 zikitolewa na kampuni za nje ya nchi kupitia kibali maalum kinachotolewa na Tume ya Madini na kwa upande wa ajira katika migodi ya madini asilimia 97 ni watanzania huku raia wa kigeni wakiwa ni asilimia (3) tatu. “Mchango wa Sekta ya Madini kweye Pato la Taifa uliongezeka kutoka asilimia 4.4 mwaka 2017 hadi asilimia 9.1 mwaka 2022; tumejipanga kuhakikisha tunavuka lengo lililowekwa la asilimia 10 kabla ya mwaka 2025,” amesema Mhandisi Samamba. Katika kikao hicho mbali na kujadili, kutatua changamoto mbalimbali katika Sekta ya Madini na kuweka mikakati ya baadaye, wajumbe wamepata fursa ya kupata elimu kutoka kwa wataalam kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)

“SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA MAZURI KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI” – MHANDISI SAMAMBA Read More »

TUME YA MADINI YAFANYA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA MADINI

Miaka mitatu ya Rais Samia………. Masoko ya madini 42 na vituo vya ununuzi wa madini 99 vyaanzishwa hadi sasa Kasi ya utoaji wa leseni za madini yaongezeka kutoka 5094 mwaka 2018/19 hadi 9,642 mwaka 2022/23 Makusanyo yaongezeka mara tatu kutoka Shilingi bilioni 213.3 mwaka 2016/17 hadi Shilingi bilioni 677.7 mwaka 2022/23 Ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi, juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanywa na Serikali ikiwa ni pamoja na kufanya Marekebisho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Mabadiliko hayo yalifanyika Mwaka 2017 yalipelekea kuanzishwa kwa Tume ya Madini na kuvunja Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na TANSORT. Akielezea uanzishwaji wa Tume ya Madini kwa kifupi Katibu Mtendaji wa Tume, Mhandisi Yahya Samamba anaeleza kuwa, Tume ya Madini ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa mwaka 2017 lengo likiwa ni kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa Sera na Sheria ya Madini ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali. Akielezea majukumu ya Tume ya Madini kwa ujumla wake, Mhandisi Samamba anafafanua ni pamoja na kutoa na kusimamia leseni za madini, kusimamia shughuli za utafutaji, uchimbaji, na biashara ya madini, kusimamia ukaguzi wa migodi na mazingira kwa ujumla. Mbali na kupongeza juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhandisi Samamba anaeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa Tume ya Madini wananchi wengi wameshuhudia mabadiliko makubwa kwenye Sekta ya Madini na kuongeza imani kwa Rais na Serikali kwa ujumla. Akielezea hali ya ukusanyaji wa maduhuli kabla na baada ya kuanzishwa kwa Tume, Mhandisi Samamba anaeleza kuwa ukusanyaji wa maduhuli umeongezeka kutoka shilingi bilioni 213.3 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 hadi shilingi bilioni 677.7 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023. “Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 kama Tume ya Madini tulipewa lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 822 na kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 677.7 ikiwa ni (82.45%) na katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 tumepewa lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 882 ambalo ninaamini kabisa tutalivuka,” anasisitiza Mhandisi Samamba. Mhandisi Samamba anasema siri ya mafaniko kwenye ukusanyaji wa maduhuli ni pamoja na uzalendo na ubunifu wa watumishi wa Tume ya Madini Makao Makuu, Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa, Maafisa Migodi Wakazi na ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Madini. Katika hatua nyingine akielezea masoko ya madini yaliyoanzishwa nchini, Mhandisi Samamba anasema kuwa masoko yalianzishwa kama njia mojawapo ya kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata soko la uhakika la madini yao baada ya kuchimba, Serikali kupata mapato na takwimu sahihi za madini yanayozalishwa na wachimbaji wadogo wa madini, kuuza madini kulingana na bei elekezi inayotolewa na Tume ya Madini kulingana na soko la dunia. Vilevile kudhibiti utoroshaji wa madini kwa wachimbaji na wafanyabiashara wasio waaminifu. Anaendelea kusema kuwa mpaka sasa Tume ya Madini ina masoko ya madini 42 na vituo vya ununuzi wa madini 99 nchini ambayo yameongeza mchango wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye mapato kutoka asilimia tano (5) hadi asilimia arobaini (40) Mwaka 2022/2023. Anasisitiza kuwa masoko ya madini yamepunguza kwa kiasi kikubwa kasi ya utoroshaji wa madini pamoja na kuleta ushindani kwa wafanyabiashara wa madini kupitia masoko na vituo vya ununuzi wa madini. Akielezea mikakati ya Serikali katika udhibiti wa utoroshaji wa madini na kuhakikisha thamani ya madini ya tanzanite inazidi kuimarika, Mhandisi Samamba anasema kuwa mnamo mwaka 2018 Serikali iliamua kujenga ukuta wa Mirerani uliopo Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa wachimbaji wa madini hayo na Serikali kwa ujumla. Anaeleza kuwa mikakati mingine iliyowekwa na Serikali ni pamoja na kuwahamisha wafanyabiashara wa madini kutoka jijini Arusha hadi Mirerani lengo likiwa ni kuinua uchumi wa eneo la Mirerani na kudhibiti utoroshaji wa madini. Aidha, anasimulia kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini inaandaa mfumo maalum wa kudhibiti mnyororo mzima wa madini ya tanzanite kuanzia kwenye uchimbaji, biashara, uongezaji thamani hadi usafirishaji wake lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa thamani ya madini hayo inazidi kupaa duniani. Katika hatua nyingine akielezea namna serikali inavyosimamia suala la ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini anasema kuwa kwa kutambua umuhimu wake, mwaka 2018 serikali iliweka kanuni na miongozo mbalimbali ya kuhakikisha watanzania wanashiriki katika shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini kupitia utoaji wa huduma mbalimbali kwenye migodi ya madini kama vile usafiri, bidhaa za kilimo, ulinzi, bima, sheria, benki, n.k. Anasema mpaka kufikia mwaka 2022 asilimia 86 ya bidhaa na huduma zinatolewa na kampuni za kitanzania kwenye kampuni kubwa za uchimbaji wa madini huku asilimia 14 zikitolewa na kampuni za nje ya nchi kupitia kibali maalum kinachotolewa na Tume ya Madini na kwa upande wa ajira katika migodi ya madini asilimia 96 ni watanzania huku raia wa kigeni wakiwa ni asilimia (4) nne “Ieleweke kuwa hakuna kampuni yoyote inayoruhusiwa kuagiza bidhaa au huduma kutoka nje ya nchi bila kupata kibali kutoka Tume ya Madini, lengo letu ni kuhakikisha kila mtanzania ananufaika na Sekta ya Madini,” anasisitiza Mhandisi Samamba. Katika hatua nyingine Tume ya Madini imekuwa ikisimamia kwa makini katika kuhakikisha kampuni za uchimbaji wa madini zinatoa huduma kwa jamii (CSR) inayozunguka machimbo yake kama Sheria ya Madini inavyoelekeza. Mhandisi Samamba anadokeza kuwa katika mafanikio kwenye Sekta ya Madini suala la usalama kwenye migodi haliwezi kuachwa nyuma, na katika kutambua hilo Tume ya Madini kupitia Kurugenzi ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira imekuwa ikifanya kaguzi za mara kwa mara kwenye migodi ya madini pamoja na kutoa elimu. Anaendelea kutaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na ongezeko la utoaji wa leseni za madini kutoka leseni 5094 katika mwaka wa fedha 2018/2019 hadi leseni 9642 katika mwaka wa fedha 2022/2023. Anaongeza kuwa mchango wa Sekta ya Madini kweye Pato la Taifa uliongezeka kutoka asilimia 4.4 mwaka 2017 hadi asilimia 9.1 mwaka 2022. Mhandisi Samamba anahitimisha kwa kusema kuwa kampuni nyingi za kigeni zimeendelea kuonesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza fursa zilizopo nchini.

TUME YA MADINI YAFANYA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA MADINI Read More »

WAZIRI MAVUNDE AONGOZA IFTAR YA TUME YA MADINI

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde akiambatana na uongozi wa Tume ya Madini ameongoza Iftar iliyofanyika jijini Dodoma. Viongozi wengine walioshiriki katika Iftar hiyo ni pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Festus Mbwilo, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Eng. Yahya Samamba, Wakurugenzi, Mameneja, Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa na watumishi wa Tume ya Madini. Akizungumza kwenye Iftar hiyo iliyoambatana na kuwaaga Makamishna wa Tume ya Madini wanaomaliza muda wao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula Waziri Mavunde amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Madini na Makamishna walioleta mageuzi makubwa kwenye Sekta ya Madini, ikiwa ni pamoja na ongezeko la makusanyo ya maduhuli la kila mwaka pamoja na kuwa na vyanzo vile vile vya makusanyo. ” Tunawashukuru sana kwa mageuzi makubwa ambayo yamefanyika katika Sekta ya Madini, majina yenu tutayaandika kwa wino wa dhahabu,” amesema Waziri Mavunde. Katika hatua nyingine sambamba na kuwapongeza watumishi wa Tume ya Madini kwa mchango mkubwa kwenye uchumi wa madini amewataka kuendelea kuimarisha umoja, kufanya kazi kwa uzalendo na ubunifu ili kuendelea kuinua Sekta ya Madini. Amesema kuwa Wizara ya Madini itaendelea kutoa ushirikiano na kutatua changamoto mbalimbali kwenye Sekta ya Madini. Wakati huo huo Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula amepongeza kwa ushirikiano mkubwa ambao umekuwa ukitolewa na Wizara ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini sambamba na kutatua changamoto mbalimbali. Katika hatua nyingine, Profesa Kikula amewataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu na ubunifu ili Sekta ya Madini iendelee kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa Pato la Taifa. Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Eng. Yahya Samamba amempongeza Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula kwa usimamizi mzuri wa Tume hali iliyopelekea kuteuliwa kwa awamu ya Pili na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Amesema kuwa, chini ya uongozi wa Profesa Kikula mabadiliko makubwa yalipatikana ikiwa ni pamoja na ongezeko la ukusanyaji wa maduhuli kwa kila mwaka, mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa kuendelea kukua, ukuaji wa Sekta ya Madini kukua, uanzishwaji wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini na ongezeko la ushiriki wa watanzania katika Sekta ya Madini kupitia maboresho ya Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini. Amesisitiza kuwa Tume itaendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa ujenzi wa ofisi mpya, usambazaji wa vitendea kazi na uboreshaji wa maslahi ya watumishi. Pia, zimetolewa zawadi kwa viongozi wa Kamisheni wanaomaliza muda wao. Awali kabla ya kuanza kwa Iftar, yamefanyika mafunzo kuhusu namna ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu kwa watumishi wa Tume.

WAZIRI MAVUNDE AONGOZA IFTAR YA TUME YA MADINI Read More »

WAZIRI MAVUNDE ANOGESHA BONANZA LA TUME YA MADINI

Aongoza kwenye mchezo wa mpira wa miguu Akabidhiwa medani ya heshima Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde leo Machi 16, 2024 kwa nyakati tofauti ameongoza timu za mpira wa miguu za Tume ya Madini Makao Makuu na Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwenye michezo ya bonanza ya Tume ya Madini iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya John Merlin jijini Dodoma. Michezo mbalimbali iliyofanyika katika bonanza hilo ni pamoja na riadha, kuvuta kamba, mpira wa miguu, kukimbiza kuku n.k. Viongozi wa Tume ya Madini walioshiriki katika bonanza hilo ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Eng. Yahya Samamba, Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa. Akizungumza kwenye bonanza hilo mara baada ya kumalizika kwa michezo mbalimbali, Waziri Mavunde amesema kuwa michezo inaimarisha umoja na kuitaka Tume ya Madini kuendelea kuboresha mabonanza mengine. Sambamba na kuwapongeza washindi wa michezo mbalimbali na kugawa vikombe, amesema kuwa kama njia mojawapo ya kuimarisha umoja katika Sekta ya Madini Wizara ina mpango wa kuandaa bonanza kubwa litakaloshirikisha Wizara ya Madini na Taasisi zake na wadau wa madini nchini. Aidha, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Tume ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini na kuongeza kuwa Wizara ya Madini itaendelea kutoa ushirikiano na kutatua changamoto zote kwenye utendaji kazi. Awali wakati akizungumza kwenye bonanza hilo, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula sambamba na kumpongeza Waziri Mavunde kwa ushiriki wa bonanza hilo amesema kuwa uongozi wa Tume umekuwa ukifanya ziara kwenye ofisi za maafisa madini wakazi wa mikoa na kutatua changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vitendea kazi na kuhamasisha umoja ili kuboresha utendaji kazi. Katika hatua nyingine, Profesa Kikula amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa hasa kwenye ukusanyaji wa maduhuli na kuongeza kuwa Tume ya Madini itaendelea kuboresha mazingira ya kazi ikiwa ni pamoja na maboresho ya ofisi na masoko ya madini. Wakati huohuo, Waziri Mavunde amekabidhiwa medani ya heshima kwa kutambua mchango wake mkubwa kwenye Usimamizi wa Sekta ya Madini na ushiriki wa bonanza ambapo amekabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula.

WAZIRI MAVUNDE ANOGESHA BONANZA LA TUME YA MADINI Read More »

Scroll to Top