Katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali madini, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 ambapo suala la Ushirikishwaji wa Watanzania lilipewa kipaumbele ili kuhakikisha Wawekezaji wote wanaojihusisha katika mnyororo wa uzalishaji na biashara ya Madini wanatoa kipaumbele kwa Watanzania nchini. Wizara ya Madini kupitia dhana ya Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri inakusudia kuiendeleza Sekta ya Madini kwa kutekeleza yafuatayo: utafiti wa jiolojia kwa njia ya high resolution airborne Geophysical Survey k… [04:10, 22/05/2024] Greyson Tume: ALIYOYASEMA WAZIRI WA MADINI, MHE. ANTHONY MAVUNDE (MB) KWENYE UFUNGUZI WA JUKWAA LA TATU LA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI JIJINI ARUSHA MEI 22, 2024 Katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali madini, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 ambapo suala la Ushirikishwaji wa Watanzania lilipewa kipaumbele ili kuhakikisha Wawekezaji wote wanaojihusisha katika mnyororo wa uzalishaji na biashara ya Madini wanatoa kipaumbele kwa Watanzania nchini. Wizara ya Madini kupitia dhana ya Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri inakusudia kuiendeleza Sekta ya Madini kwa kutekeleza yafuatayo: utafiti wa jiolojia kwa njia ya high resolution airborne Geophysical Survey katika maeneo mbalimbali nchini kutoka asilimia 16 iliyopo kwa sasa hadi kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030; kujenga maabara ya kisasa kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa miamba, udongo, maji na madini; kuanzisha makumbusho maalum ya madini; kuwawezesha wachimbaji wadogo; kuyafanya madini mkakati na madini muhimu kuwa na soko la uhakika; kuongeza thamani madini hapa nchini; kuwaendeleza wawekezaji wazawa ili kuongeza wigo wa uwekezaji unaotokana na Watanzania; kuongeza ushiriki wa Watanzania katika kusambaza bidhaa na kutoa huduma migodini; na kuandaa mazingira rafiki na kuvutia uwekezaji mkubwa kutoka nje ya nchi. “Madini ni Maisha na Utajiri”, tunamaanisha kuwa hauwezi kutenganisha maisha ya Mtanzania na Sekta ya Madini kwa kuwa kufanikiwa kwa tafiti za kina na kupatikana kwa taarifa sahihi kutachochea ukuaji wa Sekta ya Madini na kuongeza Ushirikishwaji. Usimamizi wa utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania umewezesha kuibua na kuchochea ongezeko la fursa katika nafasi za ajira na mafunzo; uhawilishaji wa teknolojia (technology transfer); utafiti na maendeleo (research and development); na matumizi ya huduma na bidhaa zinazotolewa na kuzalishwa na Watanzania. Usimamizi wa masuala ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini ni miongoni mwa majukumu ya Tume ya Madini. Utekelezaji wa jukumu hilo umekuwa na mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali, ikiwemo: kuongezeka kwa uelewa wa masuala ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini kutokana na elimu inayoendelea kutolewa na kupelekea Watanzania wengi kuona fursa mbalimbali zilizopo katika mnyororo wa thamani wa Madini. Katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024, Wizara kupitia Tume ya Madini ilipokea na kupitia jumla ya mipango 801 ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika shughuli za Madini sawa na ongezeko la asilimia 57 ikilinganishwa na mipango 510 iliyopokelewa katika kipindi kama hicho kwa Mwaka wa Fedha uliopita. Hadi kufikia Machi, 2024 jumla ya ajira rasmi 19,358 zilizalishwa katika migodi hiyo ambapo ajira 18,853 sawa na asilimia 97 zilitolewa kwa Watanzania na ajira 505 sawa na asilimia 3 zilitolewa kwa wageni. Ajira kwa watanzania kwenye migodi zitaendelea kuongezeka ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Madini Sura 123 na Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania za Mwaka 2018. Katika Mwaka 2023 kampuni za kitanzania ziliuza bidhaa na huduma migodini zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.48 ambayo ni sawa na asilimia 90 ya mauzo yote yaliyofanyika migodini yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.65. Mauzo hayo yaliyofanywa na kampuni za kitanzania kwa Mwaka 2023 yalikuwa ni zaidi ya mauzo yaliyofanywa Mwaka 2022 ambayo yalikuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.08 sawa na asilimia 86 ya mauzo yote ya Dola za Marekani bilioni 1.26. Katika kuimarisha utoaji wa huduma migodini, kampuni tatu (3) za kitanzania zimejenga viwanda vya kutengeneza vifaa vinavyotumika migodini katika eneo la Buzwagi Special Economic Zone. Kampuni hizo ni East African Conveyors Supplies Limited imejenga kiwanda cha kuzalisha conveyor belts zinazotumika kusafirisha miamba wakati wa uchakataji wa madini kilichopo Manispaa ya Kahama ambapo ujenzi wake umekamilika na wameshaanza usambazaji wa bidhaa hizo katika migodi ya ndani na nje ya nchi. Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia usimamizi wa utekelezaji wa Sheria ya Madini na kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania, kumekuwa na changamoto ambazo tukizifanyia kazi kwa pamoja zitapelekea Ushirikishwaji wa Watanzania kuongezeka na kuleta manufaa zaidi. Suala la Ushirikishwaji wa Watanzania ni takwa la kisheria na linatakiwa kuzingatiwa katika shughuli za madini na shughuli nyingine za kiuchumi. Katika kuhakikisha Watanzania wananufaika na Sekta ya Madini, Wizara kupitia Tume ya Madini itaendelea na usimamizi thabiti wa Sheria na kanuni ili kuhakikisha kuwa kipaumbele kinatolewa kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini Kupitia dhana ya Vision 2030: “Madini ni Maisha na Utajiri”, Wizara ina lengo la kukuza na kutanua wigo wa shughuli za uchimbaji Madini nchini na hivyo kuleta matokeo chanya katika ushirikishwaji wa Watanzania. Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itaendelea kuweka mazingira wezeshi na kuchochea uwekezaji wa viwanda vya uzalishaji wa bidhaa za migodini nchini ili kuwa chachu ya maendeleo endelevu ya Watanzania na Taifa kwa ujumla.