TUME YA MADINI

Taifa logo iliiyopitishwa

CONTACT US | FAQs | STAFF MAIL | ENGLISH / SWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF MINERALS

 THE MINING COMMISSION

Frequently Asked Questions

Leseni za uchimbaji wa kati wa madini (ML) hutolewa kwa kipindi kisichozidi miaka 10 na Tume ya Madini kwa Mtu/Kampuni/Ushirika katika eneo ambalo mwombaji amebaini kuwa linamfaa kuchimba baada ya kufanya utafiti. Aidha, leseni za uchimbaji mkubwa wa madini hutolewa kwa kuzingatia Kifungu cha 43 cha Sheria ya Madini Sura ya 123 ambacho kinaelekeza muda wa leseni za SML kuzingatia uhai wa mashapo au muda ulioombwa ila muda mfupi zaidi ndio utakaozingatiwa. Utaratibu na masharti ya utoaji wa leseni za uchimbaji wa kati na mkubwa wa madini ni kama inavyoelezwa:-

Utaratibu:-

1. Mwombaji kubaini eneo la leseni ya utafutaji;


2. Kujaza Fomu ya maombi na kuwasilisha Tume ya Madini Makao Makuu kwa njia ya mtandao au Hard copies;


3. Ombi kushughulikiwa, kuhakikiwa na kutathiminiwa;


4. Ombi kupendekezwa kupewa leseni kwa ML;


5. Ombi la SML kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri;


6. Ombi la SML kukubaliwa kupewa leseni;


7. Mmiliki wa Leseni kuomba ridhaa kwa mmiliki halali wa ardhi ya kuingia kwenye eneo la uchimbaji


8. Mmiliki wa leseni kuomba ridhaa ya uwekezaji kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa; na


9. Leseni kutolewa.


Masharti:-


1. Ramani: Taarifa za kijiolojia/Site Plan katika Scale ya 1:50,000;


2. Coordinates Arc, 1960 datum ya eneo linaloombwa; na Ombi liambatane na malipo ya ada;


3. Ripoti ya Upembuzi Yakinifu (Feasibility Study); na Cheti cha Mazingira (Environmental Impact Assesment – EIA) kutoka NEMC; Uthibitisho wa Utaalamu na uwepo wa fedha, Kwa ML mtaji uwe kati ya Dola za Marekani 100,000 na 100,000,000,Kwa SML mtaji usipungue Dola za Marekani 100,000,000, Mpango wa fidia na uhamishaji makazi, Mpango wa Ushirikishwaji wa Wazawa katika Mradi wa uchimbaji (Local Content Plan); na Kiapo cha Uadilifu (Integrity Pledge);


4. Letter of Offer na ada ya kuandaa leseni;


5. Idhini ya Baraza la Mawaziri;


6. Letter of Offer na malipo ya kuandaa leseni;


7. Ridhaa ya kuingia kwenye eneo;

Endapo mmiliki wa leseni hatapewa ridhaa na mmiliki wa ardhi bila sababu ya msingi, Waziri kwa kushauriana na Tume ya Madini ana mamlaka ya kumruhusu mmiliki wa leseni kuendesha utafutaji au uchimbaji wa madini (Kifungu cha 95 cha Sheria ya Madini, Sura 123);8. Ridhaa ya mmiliki wa ardhi,Leseni ya uchimbaji; na Kibali cha Mpango wa fidia kwa jamii kutoka mamlaka husika;


9. Leseni kulipiwa ada ya Mwaka.

Leseni za Uchimbaji Mdogo wa Madini hutolewa kwa kipindi kisichozidi miaka saba (7) na Tume ya Madini kwa Mtu/Kampuni/Ushirika katika eneo ambalo mwombaji amebaini kuwa linamfaa kwa shughuli za uchimbaji. Utaratibu na masharti ya utoaji wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini ni kama ifuatavyo:-


Utaratibu:

1. Mwombaji kubaini eneo linalomfaa;


2. Mwombaji kujaza Fomu ya maombi na kuwasilisha Ofisi ya Afisa Madini Mkazi kwa njia ya mtandao na Hard copies;


3. Ombi kupendekezwa na kukubaliwa kupewa leseni;


4. Mmiliki wa Leseni kuomba ridhaa kwa mmiliki halali wa ardhi ya kuingia kwenye eneo la utafutaji madini.;


5. Mmiliki wa leseni kwa kushirikiana na Mamlaka za Halmashauri/Wilaya kuandaa Mpango wa Utoaji wa Huduma kwa jamii;na


6. Leseni kutolewa .


Masharti:

1. : Ramani: Taarifa za kijiolojia/Site Plan katika Scale ya 1:50,000;

2. Coordinates Arc, 1960 Datum; Mwombaji awe Mtanzania (mtu binafsi au Kampuni) -Anuani, picha (Pasipoti) na Kitambulisho; Ombi liambatane na malipo ya Ada; Eneo lisiwe na leseni au ombi lililotangulia;


3. Mwombaji kupewa letter of Offer na kulipa ada ya kuandalia leseni;


4. Ridhaa ya kuingia kwenye eneo kutolewa endapo mmiliki wa leseni hatapewa ridhaa na mmiliki wa ardhi bila sababu ya msingi, Waziri kwa kushauriana na Tume ya Madini ana mamlaka ya kumruhusu mmiliki wa leseni kuendesha utafutaji au uchimbaji wa madini (Kifungu cha 95 cha Sheria ya Madini, Sura 123);


5. Mpango wa Huduma kwa Jamii kuandaliwa; na


6. Leseni kulipiwa ada ya Mwaka.

Leseni za Utafutaji wa Madini hutolewa kwa kipindi kisichozidi miaka minne (4) na Tume ya Madini kwa Mtu/Kampuni/Ushirika katika eneo ambalo mwombaji amebaini kuwa linamfaa kufanya utafiti. Utaratibu na masharti ya utoaji wa leseni za utafutaji wa madini ni kama Ifuatavyo:-


Utaratibu:

1. Mwombaji kubaini eneo linalomfaa kutafiti.

2. Kujaza Fomu ya Maombi na kuwasilisha Tume ya Madini kwa njia ya mtandao na Hard copies.


3. Ombi kushughulikiwa, kuhakikiwa na kutathiminiwa;

4. Ombi kupendekezwa na kukubaliwa kupewa leseni;


5. Mmiliki wa Leseni kuomba ridhaa kwa mmiliki halali wa ardhi ya kuingia kwenye eneo la utafutaji madini;


6. Mmiliki wa leseni kwa kushirikiana na Mamlaka za Halmashauri/Wilaya kuandaa Mpango wa Utoaji wa Huduma kwa jamii.; na


7. Leseni kutolewa.


Masharti

1. Sharti: Ramani: Taarifa za kijiolojia/Site Plan katika Scale ya 1:50,000;


2. Kuwasilisha Coordinates Arc, 1960 datum; Ombi liambatane na malipo ya ada; na Mtu binafsi: Jina Kamili na Uraia, Anuani ya Posta na Makazi, picha (Pasipoti) ya karibuni;


3. Kuwa na Uwezo wa Kitaalamu na Kifedha; Mwombaji asiwe na Hati ya Kosa isiyorekebishwa; Mpango wa Ushirikishwaji wa Wazawa katika Mradi (Local Content Plan); Kiapo cha Uadilifu (Integrity Pledge); Mwombaji kutomiliki leseni za utafutaji zaidi ya 20 au jumla ya ukubwa wa maeneo ya leseni za utafutaji usiozidi Kilometa za mraba 2,000; Eneo lisiwe na leseni au ombi lililotangulia;


4. Mwombaji kupewa barua ya kukubaliwa ombi (letter of offer) na kulipa ada ya kuandalia leseni.


5. Ridhaa ya kuingia kwenye eneo kutolewa.

Endapo mmiliki wa leseni hatapewa ridhaa na mmiliki wa ardhi bila sababu ya msingi, Waziri kwa kushauriana na Tume ya Madini ana mamlaka ya kumruhusu mmiliki wa leseni kuendesha utafutaji au uchimbaji wa madini (Kifungu cha 95 cha Sheria ya Madini, Sura 123).


6. Mpango wa Huduma kwa Jamii (Corporate Social Responsibility – CSR) kuandaliwa.


7. Leseni kulipiwa ada ya Mwaka.

Kuna aina 9 za Leseni ambazo hutolewa na kusimamiwa na Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini ambazo ni:

1. Leseni za Utafutaji wa Madini – Prospecting Licences (PL);

2. Leseni za Uchimbaji Mdogo wa Madini – Primary Mining Licence (PML);

3. Leseni za uchimbaji wa Kati wa Madini – Mining Licences(ML);

4. Leseni za Uchimbaji Mkubwa wa Madini-Special Mining Licences (SML);

5. Leseni za Uchenjuaji wa Madini – Processing Licence (PCL);

6. Leseni za Uyeyushaji wa Madini – SmeltingLicence (SL);

7. Leseni za Usafishaji wa Madini – Refinery Licence (RFL);

8. Leseni za Biashara Ndogo za Madini – Broker licences (BL) na

9. Leseni za Biashara Kubwa za Madini Dealer Licences (DL).

Jibu:Baada yauthamini wa madini, Tume inashirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na vyombo vya ulinzi na usalama kuhifadhi madini na utoaji wa vibalihadi kusafirishwa nje ya nchi kwenye minada mbalimbali. Aidha, Tume imeendelea na mkakati wake wa kuimairisha usimamizi wa shughuli za madini hususan kwenye maeneo ya kimikakati kama vile viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya nchi. Tume imekuwa ikishirikiana kwa karibu zaidi na vyombo vya ulinzi na usalama, uhamiaji,polisi na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na balozi za Tanzania nje ya nchi.

Jibu: Katika kuhakikisha Tume inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi na weledi mkubwa, tume ina timu ya wataalamwanaofanya kazi kulingana na muundo wa Tume.Tume ya Madini inaudwa na Makamishna nane (8); Mwenyekiti mmoja (1);Katibu Mtendaji wa Tume mmoja (1); Idara nne (4) ambazo ni Idara ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira (Mines Inspectorate and Environment Department); Idara ya Leseni na TEHAMA (Mineral Rights and Information Systems Department); Idara ya Ukaguzi na Biashara ya Madini (Mineral Audit and Trade Department); na Idara ya Huduma za Tume (Corporate Services Department); Vitengo vitatu (3) ambavyo ni Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi (Procurement Management Unit); Kitengo cha Huduma za Sheria (Legal Services Unit); na Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani (Internal Audit Unit); Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa ishirini na sita (26) – (Resident Mines Offices); na Ofisi za Madini Migodini (Mines Resident Offices).

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

Jibu: Majukumu ya Tume ni pamoja na:-

(a) Kusimamia na kuratibu kikamilifu utekelezaji wa Sheria na Kanuni za Madini;

(b) Kusimamia na kudhibiti kwa ufanisi biashara ya Madini ili kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa;

(c) Kusimamia utafutaji na uchimbaji endelevu wa rasilimali madini;

(d) Kutatua migogoro ya wachimbaji itokanayo na umiliki,utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini;

(e) Kufanya ukaguzi na uchunguzi juu ya masuala ya afya na usalama kuhusiana na shughuli za madini zinazofanyika migodini;

(f)Kuishauri Serikali katika masuala yanayohusiana na Sekta ya Madini ili kuhakikisha sheria na kanuni zote zinazohusiana na afya na usalama wa watu wanaoshiriki katika shughuli za madini;

(g)Kufuatilia na kukagua shughuli za utunzaji wa mazingira katika maeneo ya migodi na maeneo ya uchenjuaji, bajeti iliyotengwa na matumizi ya fedha kwa ajili ya ukarabati endelevu wa mazingira na ufungaji wa migodi;

(h) Kuishauri Serikali kuhusiana na masuala yoteyanayohusiana na usimamizi kwenye Sekta ya Madini kwa kuzingatia ufuatiliaji na ukaguzi wa Madini ili kuongeza mapato kwenye Sekta ya Madini;

(i) Kufanya tafiti na mipango mbalimbali itakayowezesha Sekta ya Madini kuchangia kwa ufanisi katika Pato la Taifa;

(j) Kutathmini na kufuatilia utekelezaji wa taarifa za upembuzi yakinifu za migodi, mipango ya uchimbaji, taarifa za mwaka za uzalishaji na mipango ya usimamizi na utunzaji wa mazingira migodini;

(k) Kuanzisha na kuimarisha Mfumo imara wa Ukusanyaji wa Takwimu Kitaifa kuhusiana na Madini utakaowezesha kupata taarifa muhimu na Teknolojia ya utambuzi wa Madini kwa ajili ya maslahi ya Taifa ili kuwezesha kufanya maamuzi sahihi kwenye Sekta ya Madini;

(l) Kutoa, kusitisha na kufuta leseni pamoja na vibali kulingana na Sheria na Kanuni za madini;

(m) Kufuatilia na kuhakiki uzingatiaji wa viwango vilivyowekwa katika uendeshaji wa shughuli za uchimbaji madini kwa mujibu wa Sheria, Kanunina taratibu;

(n) Kusimamia na kuhakiki kiasi na thamani ya madini yanayozalishwa na kuuzwa nje na wachimbaji wakubwa, wa kati na wadogo kwa lengo la kutathmini mapato halisi ya madini hayo na kuwezesha ukusanyaji wa mrabaha stahiki;

(o)Kukagua gharama za uwekezaji na uendeshaji wa migodi mikubwa na ya kati, kwa lengo la kukusanya taarifa sahihi za kodi na kuziwasilisha Mamlaka ya Mapato Tanzania na vyombo vingine husika vya Serikali;

(p) Kuchambua na kuthaminisha madini yaliyozalishwa na migodi mikubwa, ya kati na midogo ili kuwezesha ukusanyaji wa mrabaha stahiki;

(q) Kuandaa na kutoa bei elekezi za madini mbalimbali kutokana na bei za soko za hapa nchini na za kimataifa;

(r) Kuhakiki na kukadiria mitaji ya uwekezaji kwenye Sekta ya Madini kulingana na Kifungu cha 41 (4)(c) ya Sheria ya Madini;

(s) Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa mpango wa kuwawezesha wazawa kushiriki na kunufaika na uwekezaji katika sekta madini na utoaji huduma za kijamii kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya uchimbaji;

(t) Kutoa taarifa iwapo Tume ikiombwa kuhusiana na umiliki wa leseni au mtu yeyote anayejihusisha na shughuli za uchimbaji;

(u)Kufuatilia na kuzuia utoroshaji/magendo ya madini, na ukwepaji wa ulipaji mrabaha kwa kushirikiana na vyombo na mamlaka nyingine husika za Serikali; na

(v) Kukusanya, kuchambua, kutafsiri na kusambaza taarifa za uzalishaji na mauzo ya madini nje ya nchi kwa ajili ya maoteo ya mapato ya Serikali, kusaidia katika mipango na utoaji wa maamuzi ya usimamizi wa shughuli za madini.

Jibu Malengo makuu ya Mpango Mkakati wa Tume ni pamoja na :-

(a)Kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa Maduhuli stahiki katika sekta ya madini.

(b)Kuhakikisha Sekta ya Madini inatoa mchango mkubwa katika Pato la Taifa

(c)Kusimamia na kudhibiti biashara ya Madini ili kuongeza mchango wa Sekta ya madini katika pato la Taifa;

(d)Kusimamia na kufuatilia kikamilifu ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini na shughuli za Madini zinaendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa;

(e)Kuboresha utoaji huduma mbalimbali kwa wadau wa Sekta ya Madini;

(f)Kuimarisha mifumo ya ukaguzi na usimamizi wa migodi.

Jibu: Tume ya Madini ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa mwaka 2017 lengo likiwa ni kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa Sera na Sheria ya Madini ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali.

Scroll to Top