TUME YA MADINI

Taifa logo iliiyopitishwa

CONTACT US | FAQs | STAFF MAIL | ENGLISH / SWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF MINERALS

 THE MINING COMMISSION

WANAWAKE TUME YA MADINI WAPIGWA MSASA KUHUSU NAFASI YA TEKNOLOJIA KATIKA MALEZI YA WATOTO

Katika kuelekea kilele cha siku ya wanawake duniani, leo Machi 05, 2024 wanawake kutoka Tume ya Madini Makao Makuu na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma wamepewa mafunzo kuhusu nafasi ya teknolojia katika malezi ya watoto yaliyofanyika jijini Dodoma.

Mafunzo hayo yaliyotolewa na Daktari wa Afya ya Akili kutoka Hospitali ya Mirembe iliyopo jijini Dodoma, Sara Mwakasege lengo lake lilikuwa ni kuangalia namna ya kulea watoto katika njia bora bila kuathiriwa na mabadiliko ya teknolojia

Awali wakati akifungua mafunzo hayo Meneja wa Utawala na Rasilimali Watu wa Tume ya Madini, Fatma Chondo amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kuwajengea uwezo wa namna ya kulea familia ili kuwa na kizazi chema kwa siku za baadaye.

“ Lengo la mafunzo haya ni kuhakikisha pamoja na mabadiliko ya teknolojia bado wanawake wanakuwa mstari wa mbele kulea watoto katika malezi bora na namna ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya teknolojia,” amesema Chondo.

Kaulimbiu ya siku ya wanawake kwa mwaka huu ni “ Wekeza Kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo Ya Taifa na Ustawi wa Jamii.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top