TUME YA MADINI

Taifa logo iliiyopitishwa

CONTACT US | FAQs | STAFF MAIL | ENGLISH / SWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF MINERALS

 THE MINING COMMISSION

WAZIRI MAVUNDE ATATUA MGOGORO WA WACHIMBAJI MADINI MALERA-TARIME

 Aondoa zuio la awali la mgao wa mawe

 Aelekeza Wachimbaji waruhusiwe na mgawo kuanzia tarehe  Machi 26, 2024

 Wachimbaji waishukuru Serikali kwa utatuzi wa mgogoro na wenye Leseni za kuchimba dhahabu

 Asisitiza wachimbaji wadogo wasiondolewe katika maeneo ya uzalishaji

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde  Machi 25, 2024  alifika katika eneo la Malera Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara kwa ajili ya utatuzi wa mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wamiliki wa leseni na Kampuni ya KIRIBO ambao ulipelekea zuio la mgawo wa mawe mpaka baada ya utatuzi wa mgogoro huo.

Waziri Mavunde alitumia takribani masaa sita kutatua mgogoro husika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, watendaji wa Wizara na viongozi wa wachimbaji wadogo mkoa wa Mara (MAREMA)

“Ni maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya utatuzi wa migogoro mbalimbali katika sekta hii ya madini ambayo inadhoofisha kukua kwa uzalishaji wa madini,” alisema Mavunde

Aidha, alizipongeza  pande zote kwa kuridhia makubaliano katika hatua ya awali ya kutatua mgogoro huo.

Aliondoa  zuio la mgao wa mawe  lililokuwepo hapo awali na kuagiza mgao wa mawe kuanza  mapema Machi 26,2024. “Pia, hakikisheni katika utekelezaji wa wa maridhiano haya,  wachimbaji wadogo hawaondolewi katika eneo hilo na waachwe waendelee na shughuli zao,” alisema Mavunde.

Akitoa maelezo ya awali, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mtanda alimshukuru Waziri Mavunde kwa kufanikisha utatuzi wa mgogoro husika na kupongeza hatua za kuruhusu mgao wa mawe kwa kuwa hali ya kipato ya wananchi wa eneo hilo ilikwenda chini na mapato ya Serikali kutopatikana kwa wakati.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top