THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINING COMMISSION

WAZIRI MKUU ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI


news title here
26
Oct
2023

Leo Oktoba 26, 2023 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea banda la Tume ya Madini kwenye maonesho katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini unaotarajiwa kufungwa rasmi.

Mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa wataalam amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Tume ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini.

“ Tuna imani kubwa na hatuna mashaka na utendaji wenu kama taasisi kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini hasa katika kuhakikisha watanzania wananufaika,’ amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Awali akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Afisa Biashara wa Tume ya Madini Issa Lunda sambamba na kuelezea mikakati ya Serikali katika kuhakikisha watanzania wananufaika katika Sekta ya Madini kupitia ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini na huduma zinazotolewa na maabara ya Tume ya Madini ameongeza kuwa, kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa watanzania kwenye utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini kutokana na elimu ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara na Tume.