THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINING COMMISSION

TUME YA MADINI YAWAPIGA MSASA WADAU WA MADINI KIGOMA


news title here
06
Jun
2023

Timu ya wataalam waandamizi wa Tume ya Madini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Ukaguzi Migodi na Mazingira, Mhandisi Henry Mditi wameendelea kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini wa mkoa wa Kigoma 240 pamoja na viongozi wao kuhusu usalama, uhifadhi na usimamizi wa mazingira sambamba na masuala ya baruti katika uchimbaji mdogo wa madini.

Mada nyingine zilizotolewa katika mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba zilikuwa ni pamoja na sheria ya madini, utaratibu wa upatikanaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo wa madini, usimamizi wa mazingira migodini, biashara ya madini na ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa madini waliohudhuria mafunzo hayo wameipongeza Tume ya Madini kwa utoaji wa elimu safi na kushauri elimu kuendelea kutolewa kwenye maeneo mengine yenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini