THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINING COMMISSION

SHERIA YA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KUTALETA MATOKEO CHANYA


news title here
06
Jul
2022

Imeelezwa kuwa, endapo Sheria ya Ushiriki na Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini itasimamiwa vizuri itawezesha kufikiwa lengo la kufikia mchango wa asilimia 10 katika pato la Taifa.

Hayo, ameyasema Kamishina wa Tume ya Madini Janet Lekashingo wakati akifunga Kikao cha Chemba ya Migodi (Tanzania Chambers of Mine) na Maafisa wa Serikali kilichofanyika leo Juni 22, 2022 jijini Dodoma.

Kikao hicho kililenga kujadili juu ya utekelezaji wa Kanuni za Ushiriki na Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content), namna ya kusimamia Kanuni ya Usalama mahala pa kazi na utunzaji wa Mazingira.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho, Kamishna wa Tume ya Madini Janet Lekashingo amesema kuwa, vikao vya ushirikishwaji wa wadau ni muhimu kufanyika mara kwa mara, ambapo amesema huo ni mwanzo mzuri ili kupata urahisi wa kufanya biashara nchini ya madini nchini.

Kamishna Lekashingo ameshukuru kuwepo kwa vikao vya ushirikishwaji wa wadau wa Sekta ya Madini ambapo vinajadili mambo mbalimbali ya kueleimisha na kushauriana juu ya uwekezaji katika Sekta ya Madini.

"Tuendelee kuelimishana na kujadili vizuri kipengele kwa kipengele juu ya mada zilizowasilishwa leo, tumechukua changamoto zote tunaenda kuzifanyia kazi," amesema Lekashingo

kwa upande wake Mwenyekiti wa Chemba ya Migodi, Mhandisi Filbert Rweyemamu amesema kuwa, juhudi kwenye kuinua Sekta ya Madini inahitajika ili kuongeza thaman na ubora kwenye Sekta hiyo.

Katibu Mtendaji wa Chemba ya Migodi, Mhandisi Benjamin Mchwampaka amesema vikao kama hivyo ni vyema vikafanyika mara kwa mara kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kujadili agenda mbalimbali kuhusu Sekta ya Madini ili kupata uelewa wa pamoja.