THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINING COMMISSION

DKT. BITEKO AKABIDHI OFISI YA WIZARA YA MADINI KWA MAVUNDE


news title here
05
Sep
2023

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amekabidhi Ofisi ya Wizara ya Madini kwa Mhe. Anthony Mavunde aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Madiniili aanze rasmi kazi ya kuiongoza Wizara hiyo.

Makabidhiano hayoyalifanyika mapemaSeptemba 4, 2023 katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dodoma ambapo Dkt. Biteko alitumia fursa hiyo kumkabidhi Waziri Mavundevipaumbele vya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.

Vipaumbelevilivyowasilishwa naDkt. Biteko ni pamoja nakuimarisha ukusanyaji wa maduhuli na kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa, kuendeleza madini muhimu na madini ya kimkakati, kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini na kuhamasisha uwekezaji na biashara katika Sekta ya Madini.

Vipaumbele vingine ni uanzishwaji wa minada na maonesho ya madini ya vito, kuwaendeleza na kusogeza huduma za ugani kwa wachimbaji wadogo na kuzijengeauwezo taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Dkt. Biteko alitumia fursa hiyo kuwashukuru viongozi na watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa ushirikiano mkubwa waliomuonesha katika kipindi chake cha utekelezaji wa majukumu mbalimbali.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Anthony Mavunde alisisitiza kuwa ataonesha ushirikiano kwa watumishi wa Wizara ili kufikia malengo yaliyowekwa kwa Mwaka wa Fedha 2023/24.

Naye Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa alimshukuru Dkt. Biteko kwa ushirikiano aliompatia katika kipindi walichofanya kazi pamoja na kumtakia kheri katika majukumu yake mapya.