VIJANA 400 WAPEWA LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI WILAYANI KWIMBA MKOANI MWANZA
Posted on: July 18, 2026 10:45 | By: mwanahamisi.msangi
▪️Ni Maelekezo ya Rais Samia kufuta Leseni zisizo fanyiwa kazi na kuwapa wachimbaji wadogo ▪️Ni Leseni kubwa ya Utafiti (Ekari 5,441) iliyofutwa na kurudishwa Serikalini ▪️Waziri Mavunde aelekeza STAMICO kupeleka Mtambo wa kuchoronga Mwanza ▪️ Zoezi la Kufuta Leseni zisizofanyiwa kazi kuendelea nchi nzima Kwimba,Mwanza Serikali imeendeleza jitihada zake za kukuza Sekta ya Madini na kuwasaidia wachimbaj wadogo chini ya uongozi wa Rais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kugawa Leseni ndogo za Uchimbaji Madini (PML) kwa wachimbaji wadogo ili …
WAZIRI MAVUNDE KUWA MGENI RASMI JUKWAA LA LCCF 2026 MWANZA
Posted on: July 16, 2026 17:44 | By: mwanahamisi.msangi
MWANZA Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la Tano la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content Compliance Forum – LCCF 2026), litakalofanyika kuanzia Julai 22 hadi 24, 2026, katika Ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza. Jukwaa hilo, linaloandaliwa na Tume ya Madini, linatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini, wakiwemo makampuni ya uchimbaji wa madini, watoa huduma migodini, wafanyabiashara wa madini, taasisi za Serikali, wawekezaji pamoja na …
MAGEUZI SEKTA YA MADINI YAIFANYA TANZANIA KUWA KITOVU CHA UWEKEZAJI AFRIKA - DKT. KIRUSWA
Posted on: July 08, 2026 20:32 | By: mwanahamisi.msangi
🔶_Tume ya Madini yaeleza usimamizi wa leseni za madini na Local Content unavyowanufaisha Watanzania_ 🔶_Fursa za uwekezaji zatangazwa kuanzia utafiti, uchimbaji hadi uongezaji thamani wa madini_ 📍Dar es Salaam Serikali imesema mageuzi yanayoendelea kutekelezwa katika sekta ya madini chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yameifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye mazingira bora ya uwekezaji barani Afrika, huku ikiwakaribisha wawekezaji kuwekeza katika utafiti, uchimbaji, uchenjuaji, uchakataji na uongezaji thamani wa madini. Kauli hiyo imetolewa leo, Julai 8, …
DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050 YAIPA SEKTA YA MADINI MWELEKEO MPYA WA KUCHOCHEA UCHUMI
Posted on: July 06, 2026 18:20 | By: mwanahamisi.msangi
Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet R. Lekashingo, amesema Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 imeipa sekta ya madini nafasi ya kimkakati ya kuongoza mageuzi ya uchumi wa Tanzania kupitia uongezaji thamani wa madini, ushirikishwaji wa watanzania na matumizi ya teknolojia za kisasa katika shughuli za uchimbaji wa madini. Akizungumza mapema leo Julai 6, 2026, alipotembelea mabanda ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini katika Kijiji cha Madini kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya …
BORESHENI UTOAJI LESENI ZA MADINI KUPUNGUZA MIGOGORO - MBIBO
Posted on: July 05, 2026 16:41 | By: mwanahamisi.msangi
Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo, ameagiza Tume ya Madini kuboresha mfumo wa utoaji wa leseni za madini ili kuongeza ufanisi, kuimarisha uwazi na kupunguza migogoro katika shughuli za utafiti, uchimbaji na uchenjuaji wa madini nchini. Mbibo ametoa maelekezo hayo leo, Julai 5, 2026, alipotembelea banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. …
SABASABA YAFUNGUA FURSA MPYA ZA MADINI, WAFANYABIASHARA WAKIRI UTAJIRI MKUBWA WA TANZANIA
Posted on: July 04, 2026 12:50 | By: mwanahamisi.msangi
_Serikali yapongezwa kwa kuimarisha sekta ya madini, wawekezaji waendelea kuonesha imani kubwa_ DAR ES SALAAM Wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini wameipongeza Serikali kwa kuendelea kuimarisha usimamizi wa sekta hiyo kupitia uwazi, utekelezaji wa sheria na matumizi ya mifumo rasmi ya biashara, hatua ambazo zimeongeza imani ya wawekezaji, ufanisi wa biashara na mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa Taifa. Pongezi hizo zimetolewa na mfanyabiashara mkubwa wa madini ya Tanzanite nchini, Taikoo Kulunju Oletipa, baada ya kutembelea banda …
TANZANITE YAPAA SABASABA WANANCHI WAVUTIWA NA UPEKEE WAKE
Posted on: July 03, 2026 15:58 | By: mwanahamisi.msangi
DAR ES SALAAM Madini ya Tanzanite yameendelea kuwa kivutio kikubwa katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), huku mamia ya wananchi wakifurika katika Banda la Tume ya Madini kujionea kwa karibu jiwe hilo la thamani linalopatikana Tanzania pekee duniani pamoja na kupata elimu kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya madini. Maonesho hayo yenye kaulimbiu ya “Fahari ya Tanzania” yalianza rasmi Juni 28, 2026 na yanatarajiwa kuhitimishwa Julai 13 2026, sambamba na maadhimisho ya miaka …
WAKAGUZI WASAIDIZI WA MADINI WATAKIWA KUZINGATIA UBUNIFU NA UZALENDO KATIKA USIMAMIZI WA SEKTA YA MADINI
Posted on: June 25, 2026 17:16 | By: mwanahamisi.msangi
_Katibu Mkuu Wizara ya Madini apongeza mchango wao katika ongezeko la makusanyo ya maduhuli_ 📍MOROGORO Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, amewataka Wakaguzi Wasaidizi wa Madini nchini kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ubunifu, uzalendo na uadilifu ili kuhakikisha Sekta ya Madini inaendelea kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa. Amesema sekta hiyo ni miongoni mwa sekta zilizopewa kipaumbele katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hivyo usimamizi madhubuti wa rasilimali za madini ni …
MHANDISI SAMAMBA AWATAKA WATENDAJI WA TUME YA MADINI KUIMARISHA USIMAMIZI WA SEKTA YA MADINI
Posted on: June 24, 2026 17:22 | By: mwanahamisi.msangi
_Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa watakiwa kuharakisha utatuzi wa migogoro na kusimamia matumizi bora ya leseni za madini_ 📍MOROGORO Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, amewataka watendaji wa Tume ya Madini nchini kuendelea kuimarisha usimamizi wa Sekta ya Madini kupitia usimamizi madhubuti wa leseni za madini, utatuzi wa migogoro kwenye uchimbaji wa madini pamoja na kuongeza ushiriki wa Watanzania katika shughuli za mnyororo wa thamani wa madini ili sekta hiyo iendelee kutoa mchango mkubwa katika Pato la …