TUME YA MADINI

CONTACT US | FAQs | STAFF MAIL | ENGLISH / SWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF MINERALS

 THE MINING COMMISSION

Madini News

WAZIRI MAVUNDE AZINDUA MAGARI 25 YA TUME YA MADINI

Ni sehemu ya magari 89 na pikipiki 140 zinazotarajiwa kununuliwa Lengo kuboresha Sekta ya Madini Aagiza Magari kufungwa GPS Ampongeza Rais Samia kwa kuiongezea bajeti Wizara ya Madini DODOMA Ikiwa ni mkakati wa kuimarisha usimamizi katika Sekta ya Madini hasa kwenye ukusanyaji wa maduhuli, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amezindua magari mapya 25 kwa ajili ya kusambazwa kwenye Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa sambamba na kukabidhi magari hayo kwa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa waliohudhuria uzinduzi huo. Uzinduzi huo umehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo na watendaji wengine kutoka Wizara ya Madini na Taasisi zake. Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mhe. Waziri Mavunde amesema kuwa Wizara imepanga kununua magari 89 na pikipiki 140 kama sehemu ya uboreshaji wa usimamizi wa Sekta ya Madini kupitia Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa hasa kwenye usimamizi wa ukusanyaji wa maduhuli na kudhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato na utoroshaji wa maduhuli. Amesema kuwa, magari yaliyozinduliwa 25 ni awamu ya kwanza ya magari 89 yanayotarajiwa kuletwa sambamba na pikipiki 140 zitakazosambazwa kwenye ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa zilizopo nchi nzima. Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipa kipaumbele Sekta ya Madini kwa kuiongezea bajeti Wizara ya Madini kutoka shilingi bilioni 89 mwaka 2023/2024 hadi shilingi bilioni 231 katika mwaka wa fedha 2024/2025 “ Ongezeko hili ni dhahiri kabisa Dkt. Samia anatamani kuona Sekta ya Madini inaendelea kuimarika na mchango wake kuongezeka kwenye Pato la Taifa hasa kwenye ukusanyaji wa maduhuli, mathalan katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 tumepewa lengo la kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni Moja ambapo ndani ya siku 90 tumeweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 287 ikiwa ni asilimia 106 ya lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 249 ndani ya kipindi husika,” amesisitiza Waziri Mavunde. Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde ameelekeza magari yote kufungwa GPS kwa ajili ya kuangalia mwenendo wake ili kuhakikisha yanatumika katika matumizi yaliyokusudiwa. “Magari yote yatafungwa GPS ambapo Makao Makuu tutakuwa na uwezo wa kuona mwenendo wa magari kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini hasa kwenye shughuli za ukusanyaji wa maduhuli na ukaguzi wa migodi ya madini,” amesisitiza Waziri Mavunde. Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo amempongeza Waziri Mavunde kwa jitihada zake za usimamizi wa Sekta ya Madini na kuwataka watendaji wa Tume ya Madini kuhakikisha wanaonesha matokeo chanya kwenye utendaji kazi. Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo sambamba na kuishukuru Wizara ya Madini kwa magari husika amesema kuwa magari yatatumika kama chachu ya Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwenye ongezeko la makusanyo ya maduhuli. Amefafanua kuwa magari yote 85 yatakayonunuliwa yatagharimu zaidi ya shilingi bilioni 18.  

WAZIRI MAVUNDE AZINDUA MAGARI 25 YA TUME YA MADINI Read More »

WIZARA YA MADINI KUREJESHA MINADA YA NDANI NA KIMATAIFA MADINI YA VITO

  ●Itafanyika ndani ya nchi na nje ya nchi ●Itaendeshwa na Tume ya Madini kushirikiana na Soko la Bidhaa Tanzania ●Marekebisho ya Sheria na Kanuni yakamilika ⚫️ Ni utekelezaji wa Rais Samia kukuza biashara ya Tanzanite Dodoma Serikali kupitia Wizara ya Madini inarudisha minada ya ndani ya madini ya vito itakayofanyika katika maeneo ya uzalishaji hususan Mirerani, Mahenge, Tunduru, Dar es salaam, Arusha na Tanga na kimataifa itafanyika mji wa Bangkok na Jaipur nchini Thailand. Hayo yamesemwa leo Oktoba 16, 2024 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini jijini Dodoma. Waziri Mavunde amesema kuwa baada ya taratibu za marekebisho ya kisheria kukamilika juu ya uendeshaji wa minada hiyo wanatarajia ndani ya muda mfupi ujao kuanza taraibu za kuweka miundombinu ya kuanza minada ya ndani. Waziri Mavunde amefafanua kuwa, uendeshaji wa maonesho na minada ya kimataifa nchini ni fursa muhimu ya kutangaza madini ya vito yanayozalishwa hususan kwenye masoko ya kimataifa ambayo ni njia mojawapo ya kuwafikisha watanzania katika masoko ya uhakika na upatikanaji wa bei nzuri na stahiki. Waziri Mavunde ameieleza Kamati ya Nishati na Madini kuwa, Mpango wa kurejesha minada ya madini ya vito ni utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha kusafisha dhahabu cha jijini Mwanza tarehe 13 Juni, 2024. Kwa upande wake , Naibu Waziri wa madini Dkt.Steven Kiruswa amesema, kwa sasa wataalam wa Wizara ya Madini wamepata uzoefu mkubwa katika minada na maonesho ya kimataifa baada ya kujifunza namna biashara za kimataifa zinavyofanyika pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa kwenye mnyororo mzima wa thamani madini katika nchi mbalimbali ikiwemo Marekani , India , Afrika Kusini na Thailand. Awali, akiwasilisha taarifa kuhusu uboreshaji na utekelezaji wa Kanuni za Usimamizi wa Masoko na vituo, minada ya ndani na kimataifa ya madini ya vito kwa Kamati hiyo, Kaimu Mtendaji Tume ya Madini Mhandisi Ramadhani Lwamo amesema kuwa, minada hiyo itaendeshwa na Tume ya Madini kwa kushirikiana na Soko la Bidhaa la Tanzania (TMX) kupitia mfumo wa mauzo wa kielektroniki ambapo usimamizi utahusisha shughuli za uthaminishaji na upangaji wa madini ili kuweza kupata bei nzuri kulingana na madini husika,akisisitiza kwamba lengo kuu ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara ya madini ya vito na usonara barani Afrika. Mhandisi Lwamo ameongeza kuwa, minada ya vito itaifungamanisha Sekta ya Madini na Sekta nyingine za kiuchumi ikiwemo Utalii na biashara katika kipindi husika ikiwa ni pamoja na kuliingizia taifa fedha za kigeni. Pamoja na mambo mengine, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt. David Mathayo ameendelea kumpongeza Waziri wa Madini na wasaidizi wake kwa kazi nzuri ya kuisongesha Sekta ya Madini katika ngazi ya kimataifa inayoleta tija katika uchumi wa nchi na hasa katika mkakati wa kurudisha hadhi na thamani ya madini ya vito yakiwemo madini ya Tanzanite ambayo ni madini yanayopatikana Tanzania peke yake.  

WIZARA YA MADINI KUREJESHA MINADA YA NDANI NA KIMATAIFA MADINI YA VITO Read More »

RAIS SAMIA AIPONGEZA WIZARA YA MADINI KWA USIMAMIZI MADHUBUTI WA SEKTA

  ⚫️ Trilioni moja yatengwa kwa ajili ya ununuzi wa dhahabu kupitia BOT ● Shilingi Bilioni 250 zatengwa kama dhamana ya mikopo kwa wafanyabiashara wa dhahabu ●Mwaka 2023 madini yenye thamani zaidi Trilioni mbili yaliuzwa kupitia masoko ●Serikali kuongezea mitambo ya uchorongaji 10 zaidi kwa ajili ya wachimbaji wadogo GEITA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia S. Hassan kwa usimamizi madhubuti wa sekta unaopelekea ukuaji wa haraka wa mchango wa sekta ya madini katika pato la Taifa. Hayo yameelezwa leo Oktoba 13, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akifunga maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita. Aidha Mh Rais Samia ameeleza katika mikakati ya kuimarisha uchumi wa nchi na upatikanaji wa fedha za kigeni Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetenga kiasi cha shilingi Trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dhahabu kutoka kwa wachimbaji. Rais, Dkt. Samia amesema kwamba sekta ya madini imekuwa na mchango mkubwa katika kuliingizia taifa fedha za kigeni ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ilichangia asilimia 56 ya fedha za kigeni. Sambamba na hapo Rais , Dkt.Samia amesema kiasi cha shilingi 250 zimetengwa kama dhamana ya mikopo zitakazo wawezesha wanunuzi wa dhahabu kupata mtaji. Rais Dkt. Samia amesema kuwa , kwa mwaka wa 2023 mauzo ya madini yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni mbili yaliuzwa katika masoko 44 na vituo mbalimbali vya uuzaji madini vilivyopo sehemu mbalimbali nchini. Akielezea kuhusu mwenendo wa biashara ya madini nchini kuanzia mwaka 2019 mpaka septemba 2024 , Dkt.Samia amesema kwa kipindi husika kiasi cha tani 20.8 za dhahabu zenye gharama ya shilingi trilioni 5.2 zimenunuliwa kutoka kwa wachimbaji na wafanyabiashara ya madini nchini. Dkt.Samia ameeleza serikali inatambua mchango wa asilimia 40 kutoka kwa wachimbaji wadogo nchini, ambapo ametoa leseni 21 kwa vikuandi vya Vijana na wanawake vikiwemo vikundi vya GEWOMA , Ushirika Madirisha na TEWOMA vinavyojihusisha na uchimbaji mdogo. Naye , Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt.Dotto Biteko ameipongeza wizara ya madini kwa juhudi mbalimbali inazofanya za mageuzi katika mnyororo wa thamani katika sekta ya madini hususan katika masuala uongezaji thamani madini na mpango ya kufanya utafiti wa kina kwa asilimia 50 ifikapo mwaka wa 2030. Akielezea kuhusu mikakati iliyopo ndani ya sekta ya madini , Waziri wa Madini , Mhe. Anthony Mavunde amesema katika kuimarisha uchimbaji wenye tija na uhakika Serikali itajenga Maabara kubwa mkoani Dodoma na Geita ili kuwawezesha wachimbaji wadogo kupeleka sampuli zao kwa ajili ya uchunguzi wa sampuli za madini na miamba. Waziri Mavunde amesema kuwa wizara inaendelea kuweka mipango mizuri katika ukusanyaji wa maduhuli ambapo kwa kipindi cha siku 90 cha mwaka wa 2024/2025 wizara kupitia Tume ya Madini imekusanya kiasi cha shilingi Bilioni 287 ambayo ni zaidi ya asilimia 106. Akielezea kuhusu utekelezaji wa Sheria na Kanuni ndani ya Wizara, Waziri Mavunde amesema kuwa wizara imekuwa ikizingatia taratibu zote za utekelezaji wa Mpango wa Ushirikishwaji wa Jamii inayozunguka mgodi na Mpango wa Urudishaji kwa Jamii ambapo kwasasa ipo na mpango mpya wa Mining for Brighter Tommorrow (MBT) utakao washirikisha vijana na wakina mama. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mhe. Constantine Kanyasu amemshukuru Rais , Dkt.Samia kwa kupeleka fedha za miradi ya maendeleo mkoani Geita katika sekta ya Afya,Maji, Barabara na Elimu. Pamoja na mambo mengine , Rais wa Shirikisho la Wachimbaji wadogo wa madini Tanzania (FEMATA) John Bina amemuomba Rais , Dkt. Samia kuifanya dira ya Vision2030 ya Madini ni Maisha na Utajiri kuwa kitaifa badala ya kisekta. Kwa mara ya kwanza maonesho ya Saba ya Teknolojia ya madini yamefungwa leo rasmi na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

RAIS SAMIA AIPONGEZA WIZARA YA MADINI KWA USIMAMIZI MADHUBUTI WA SEKTA Read More »

MAONESHO YA MADINI GEITA KUBORESHWA KUFIKIA HADHI YA KIMATAIFA-MAVUNDE

  -Rais Samia Suluhu Hassan kufunga maonesho -Idadi ya washiriki wa nje ya nchi waongezeka -RC Shigela aeleza mpango wa kujenga majengo ya kudumu na kuboresha miundombinu 📍Bombabili EPZ, Geita Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amepongeza maonesho ya 7 ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita kwa kuendelea kukua na kuongeza idadi kubwa zaidi ya washiriki wa ndani na nje ya nchi na hivyo kufikisha idadi ya zaidi ya washiriki 800 kwa mwaka huu 2024 na hivyo kuutaka mkoa wa Geita kuimarisha miundombinu ya eneo la Maonesho ili kuyafanya ya Kimataifa. Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Geita,wakati akikagua maonesho na kutoa hati za pongezi,ushiriki na ushindi kwa waoneshaji wa bidhaa na huduma. “Ni dhamira ya Serikali kuona maonesho haya yanakuwa na kufikia hadhi ya kimataifa,hivyo Wizara ya Madini na Mkoa wa Geita tutashikiriana kwa ukaribu ili azma na ndoto hii kutimia. Maonesho ya mwaka huu yamevutia udhamini mkubwa na ushiriki wa wadau wengi sana wa nje na ndani ya nchi,na hii ni dalili njema ya ukuaji wa maonesho haya mwaka hadi mwaka”Alisema Mavunde Akitoa salamu zake,Mkuu wa Mkoa wa Geita amewapongeza washiriki wote wa mwaka huu kwa kuwa mahiri na wabunifu na hivyo kuyafanya maonesho haya kuvutia watu wengi wakiwemo wageni kutoka nchi mbalimbali. Mh Shigela pia ameeleza mkakati wa mkoa ni kujenga miundombinu ya kudumu na kuboresha eneo la maonesho ili kukidhi mahitaji ya kimataifa. Maonesho haya ya 7 ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita yanafikia tamati tarehe 13.10.2024 kwa kuhitimishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia S. Hassan ambaye anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.

MAONESHO YA MADINI GEITA KUBORESHWA KUFIKIA HADHI YA KIMATAIFA-MAVUNDE Read More »

ZAIDI YA ASILIMIA 90 YA WATOA HUDUMA MIGODINI NI WATANZANIA – LWAMO

  – Awaasa vijana kutunza afya, kuwa waaminifu – Awataka kujiepusha na migogoro isiyo na tija Azindua mkutano wa umoja wa vijana migodini Mwandishi Wetu Zaidi ya asilimia 90 ya huduma zinazotolewa kwenye migodi ya madini nchini zinatolewa na watanzania huku vijana wakiaswa kutunza afya zao na kuepuka makundi hatarishi ili kuzifikia fursa zilizopo kwenye migodi. Hayo yamesemwa leo Oktoba 7, 2024 na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo wakati akimwakilisha Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde kwenye ufunguzi wa kongamano la mafunzo ya fursa katika Sekta ya Madini kwa vijana sambamba na umoja wa vijana wa migodini (Tanzania Youth in Mining), kwenye ukumbi wa EPZA uliopo viwanja vya Bombambili ambako Maonesho ya Saba ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Geita yanayoendelea. Mhandisi Lwamo amesema, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imekuwa kinara kuhakikisha makundi yote yanashiriki ipasavyo katika Sekta ya Madini ambapo imekua ikitoa leseni za uchimbaji wa madini, vibali vya huduma kwenye migodi ‘local content’ na kuongeza kuwa mpaka sasa hivi zaidi ya asilimia 90 ya watoa huduma ni watanzania. Amesema, Taifa lolote ili liendelee linapaswa kuwa na vijana wenye malengo na tija na kuwataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika Sekta ya Madini ikiwemo fursa katika uchimbaji, fursa za biashara na watoa huduma migodini ‘Local Content’. “Fursa kama hizi ili muweze kuzifikia ni lazima muwe kwenye vikundi na Serikali kupitia vikundi vyenu itaweza kuwafikia na kutimiza lengo la vijana na kukuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla,”amesema na kuongeza “Vijana, jambo kubwa na la msingi niwaase ili kufikia ndoto zenu ni lazima mtunze afya zenu, mnaweza kuwa na ndoto kubwa za mafanikio lakini kama afya zenu mnachukulia mzaha mzaha hamtazitimiza tunzeni afya,”amesisitiza Mhandisi Lwamo. Pia, amewaasa kuwa waaminifu kwa kuwa vikundi vingi vya vijana vinakufa kutokana na kukosa uaminiufu. “Tumeona vikundi vingi vinavurugika wakati mwanga umeanza kuchomoza, mmetoka kwenye shida, imefikia wakati wa kupata faida mnaanza kuleta vurugu kwenye vikundi, hatutaki vijana ambao mna ndoto kubwa ya kutufikisha kwenye ‘Vision ya 2030’ ya Madini ni Maisha na Utajiri mkaishia njiani, kwa kuingiza tamaa, kutokuaminiana ambako huzaa vurugu zisizo na faida,”amesema Mhandisi Lwamo. Aidha, amesema Serikali siku zote imekuwa ikitoa kipaumbele kwa vijana kuhakikisha inaendelea kutoa leseni kwa wachimbaji vijana ili wanufaike na rasilimali madini na kwamba ili kuendelea kama taifa, kuna vitu vya msingi ambavyo vitapaswa kuzingatiwa ikiwemo kutunza na kuendeleza maliasili ambazo Mwenyezi Mungu ametujalia. “Tutaziendeleza kwa kuwa na elimu ya kutosha ya kuendesha rasilimali hizi kibiashara, hivyo tumieni fursa za elimu ya ujasiriamali ili muweze kufikia ndoto zenu kwa kunufaika na maliasili zilizopo. “Sio wote mtachimba, naamini wapo wenye vipaji vya uchimbaji, wengine biashara, kusambaza baruti, wengine uchenjuaji wa dhahabu au madini yatakayopatikana, kila mtu ajiangalie kipaji alichonacho akifanyie kazi kwa kuchangamkia fursa, Tume tupo kuwapa mwongozo ili mfikie ndoto zenu, hivyo zingatieni mafunzo mtakayopewa hapa hakikisheni hamtoki bure,”amesema Lwamo. Awali akizungumza, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Madini Taifa, Hamis Mohamed amesema umoja huo uliundwa kwa maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Rais Samia aliagiza tuunde umoja ili changamoto zetu ziweze kutatuliwa kwa urahisi pia tupate sehemu ya kusemea vitu vinavyotuhusu kama vijana katika Sekta ya Madini ikiwemo kusaidiwa kuzifikia fursa mbali mbali zilizopo,”amesema Hamis na kuongeza “Wachimbaji vijana tuna changamoto nyingi, Serikali haiwezi kututatulia changamoto zetu zote, zipo kupitia umoja wetu tunakabiliana nazo na kuzitatua sisi wenyewe,”amesisitiza. Uzinduzi wa umoja huo wa vijana umekwenda sambamba na mafunzo ambayo yametolewa na Mtaalam kutoka Tume ya Madini, Mjiolojia John Maganga ambaye alimwakilisha Afisa Madini Mkazi wa Geita, Samwel Shoo, ambapo amezungumzia fursa za kiuchumi, maadili kwa vijana na kwamba dhamira ya Serikali ni kuboresha maisha katika Sekta ya Madini.

ZAIDI YA ASILIMIA 90 YA WATOA HUDUMA MIGODINI NI WATANZANIA – LWAMO Read More »

WIZARA YA MADINI TUMEFIKIA MUAFAKA KATIKA KUTENGA 20% YA UZALISHAJI WA DHAHABU BOT

Ninawashukuru sana wadau wa Madini,Wachimbaji wakubwa,kati,wadogo na Wafanyabiashara ya Madini ambao kupitikia kikao cha pamoja katia yao na Benki kuu ya Tanzania (BOT) na Wizara ya Madini tumefikia muafaka katika maeneo mengi na hivyo kuwezesha utekelezaji wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini juu ya kutenga 20% ya uzalishaji wa dhahabu kwa ajili ya akiba ya nchi kupitia BOT. MAMBO MUHIMU i. Bei: Bei itakayotumika ni bei ya dhahabu duniani kama inavyotolewa na Tume ya Madini, hivyo bei hubadilika kila siku; ii.Malipo: Asilimia 100 ya malipo baada ya kupokea ripoti ya uchenjuaji wa dhahabu; iii. Muda wa malipo: Ndani ya masaa 24 baada ya kupata ripoti ya uchenjuaji. Kwa miamala ya tarehe 02 Oktoba 2024, malipo yalifanyika ndani ya masaa sita; iv. Gharama za kuchenjua: Benki Kuu italipia asilimia 100 ya gharama za kuchenjua dhahabu; v. Asilimia 20 ya dhahabu: Hii inahusu mmiliki wa leseni ya chimbaji wa madini na mfanyabiashara mkubwa wa madini; vi. Motisha: Mrabaha asilimia 4 badala ya asilimia 6; Ada ya ukaguzi ni asilimia 0 badala ya asilimia 1; na Kodi ya Ongezeko la Thamani asilimia 0, hivyo muuzaji wa dhahabu anaweza kudai “input tax” vii. Chini ya mpango huu, wamiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini, wafanyabiashara wakubwa wa madini na viwanda vya kuchenjulia dhahabu wanaweza kuluzia Benki Kuu kiasi chochote cha dhahabu. Anthony Peter Mavunde Waziri wa Madini 7.10.2024

WIZARA YA MADINI TUMEFIKIA MUAFAKA KATIKA KUTENGA 20% YA UZALISHAJI WA DHAHABU BOT Read More »

KAMPUNI YA GEITA RESOURCES LIMITED YANADI FURSA

Vipo vifaa vya kisasa vya uchimbaji madini GEITA Kampuni ya Geita Resources Limited inayojihusisha na utafiti, uchimbaji wa madini ya dhahabu, uuzaji wa kemikali za kuchenjua dhahabu na usambazaji wa vifaa vya uchimbaji wa madini kwenye Sekta ya Madini imekaribisha wadau wa madini na wananchi kwa ujumla kujifunza na kujionea vifaa vya kisasa vya uchimbaji wa madini. Akizungumza kwenye mahojiano maalum, mtaalam kutoka kampuni hiyo, John Sililo leo Oktoba 7, 2024 kwenye Maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini katika Viwanja vya Bombambili mkoani Geita, amesema kuwa kampuni hiyo iliyoanzishwa tangu mwaka 2022 ilianza kutumia teknolojia ya kizamani katika kukamata dhahabu (Metal detector) ambapo kwa sasa wanatumia teknolojia ya kisasa zaidi ya (Shaking table/washing plant) ambayo inatumika kuzalisha dhahabu za vikole. Katika hatua nyingine, Sililo ameishukuru Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kwa miongozo na maelekezo kwa wachimbaji wadogo hususan katika masuala ya kiusalama ambapo Tume ya Madini imekuwa ikiwatembelea na kuangalia usalama wa maeneo mara kwa mara sambamba na kutoa elimu kuhusu usalama kwenye shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini. Vilevile amesema kuwa, wameweza kupiga hatua kutoka uchimbaji mdogo na kuwa wachimbaji wa kati, ambapo walikuwa wanachimba kwa kutumia duara za matimba na sasa wamefikia hatua ya kuchimba kwa kutumia duara za zege (Concrete Shaft) ambazo zinadumu mpaka miaka 100. “Kutokana na jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alizozifanya kwenye Sekta ya Madini tumeweza kunufaika kwa kupelekewa nishati ya umeme kwenye maeneo ya uchimbaji ambapo imepunguza gharama za uzalishaji Akieleza mipango ya Kampuni amesema kwa sasa wanaajiri watu wenye uzoefu katika masuala ya Utafiti, Uchimbaji na Uchenjuaji kwa lengo la kuongeza uzalishaji na kutengeneza ajira nyingi kwa Watanzania pamoja na kuendelea kuongeza migodi katika mikoa mingine. Ameongeza kuwa, wana Ofisi katika mikoa ya Geita, Mwanza, Simiyu, na Tabora na wanapatikana kwa mawasiliano ya namba za simu +255742333345/0764 570579 na www.geitaresource.com

KAMPUNI YA GEITA RESOURCES LIMITED YANADI FURSA Read More »

NAIBU WAZIRI MKUU BITEKO AIPONGEZA WIZARA YA MADINI KWA MPANGO WA KUONGEZA AKIBA YA DHAHABU NCHINI

-Awataka wadau kuunga mkono mpango wa Serikali -Waziri Mavunde asema mgomo umeisha kupitia mariadhiano -BOT yaendelea kununua dhahabu kwa bei ya soko -Wadau watoa kauli ya kuunga mkono mpango wa serikali 📍 Bombambili,Geita Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Mashaka Biteko ameipongeza Wizara ya Madini kwa mkakati wanaoutekeleza ambao unawazesha upatikanaji wa akiba ya Dhahabu kupitia Benki kuu ya Tanzania jambo ambalo ni muhimu kwa maendeleo ya Uchumi wa Tanzania. Hayo yamesemwa jana Oktoba 05 2024 wakati wa ufunguzi wa maonesho ya saba ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yenye kauli mbiu ya “Matumizi ya Teknolojia sahihi ya Nishati safi katika sekta ya Madini kwa maendeleo endelevu” yanayofanyika Mkoani Geita. “Sisi utajiri ambao Mungu ametujaalia ni utajiri wa madini ikiwemo Dhahabu, lazima madini haya yawe chachu katika ukuaji wa uchumi wetu. Naipongeza Wizara ya Madini kwa bidii kubwa mlioifanya sasa ya kuanzisha na kusukuma uwepo wa akiba ya Dhahabu kupitia Benki kuu ya Tanzania”, alisema Mh. Biteko. Kwa upande wake Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameeleza kwamba kwa sasa baada ya kukaa pamoja baina ya serikali na wadau wamefikia muafaka na hakuna mgomo tena wa kutoiuzia Dhahabu BOT baada ya ufafanuzi wa baadhi ya hoja na elimu kutolewa ikiwa ni sehemu ya falsafa ya maridhiano inayohubiriwa kwa nguvu na Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan. Mh Mavunde ametoa rai kwa wadau wote kushirikiana na serikali katika mpango huu wa upatikanaji wa akiba ya dhahabu kupitia BOT na kuahidi kutoa ushirikiano katika kushughulikia changamoto mbalimbali zitakazojitokeza. Akitoa maelezo ya awali, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kukuza Sekta ya Madini hasa kwa Wachimbaji wadogo na kuahidi kwamba Mkoa wa Geita utaendelea kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya madini ambapo mkoa huo ni mzalishaji mkubwa wa madini ya dhahabu. Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Kilumbe Shabani Ng’enda ameeleza kuwa Kamati inaridhishwa na mwenendo wa Wizara ya madini hususani inavyosimamia sheria na sera ya madini kwa manufaa ya uchumi wa watu na nchi kwa ujumla. Akitoa salamu zake,Rais wa Shirikisho la Vyama cha Wachimbaji Madini(FEMATA) Ndg. John W. Bina ameipongeza Wizara ya madini kwa usikivu na majadiliano ya mara kwa mara pindi changamoto zinapojitokeza na kuahidi kwamba baada ya kikao cha pamoja wadau wameridhia mpango wa serikali wa ununuzi wa dhahabu kupitia BOT.  

NAIBU WAZIRI MKUU BITEKO AIPONGEZA WIZARA YA MADINI KWA MPANGO WA KUONGEZA AKIBA YA DHAHABU NCHINI Read More »

RC SHIGELLA ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI

Dkt. Biteko kufungua Maonesho ya Madini Geita – RC Shigella atembelea Banda la Tume ya Madini Mwandishi Wetu NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko atazindua Maonesho ya Saba ya Kitaifa ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Geita yaliyoanza Oktoba 2, kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita. Akizungumza katika Banda la Tume ya Madini Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigella ambae aliongozana na Afisa Madini Mkazi wa Geita, Samwel Shoo, amesema mwaka huu kuna washiriki zaidi ya 600. Amesema, Maonesho ya mwaka huu yatakua na washiriki kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Congo, Rwanda, Burundi na Kenya. “Ni fursa kwa wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa, watumie maonesho haya kuja kujifunza teknolojia mbali mbali ya sekta ya madini, kuna Banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake ikiwemo Tume ya Madini hivyo watanzania wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya madini watembelee mabanda haya kujifunza na kupata elimu katika mnyororo mzima wa sekta ya madini,” amesema Mhe. Shigella. Aidha, amewataka wachimbaji kujifunza Teknolojia ya utafiti wa madini katika hekari 120 na 130 na kwamba ukifanya utafiti lazima utumie teknolojia ya bei ya rahisi uweze kujua madini yanapatikana wapi na kwa kiasi gani. Amesema pia watajifunza Teknolojia ya uchimbaji wa gharama nafuu ili mchimbaji asiingie gharama kubwa katika uchimbaji. Pia watajifunza suala zima la uchenjuaji madini kutoka kwenye mawe, mchanga au udongo ikiwa ni pamoja na uongezaji thamani wa dhahabu ili wananchi wapate dhahabu asilimia 90 ikiwa haijachanganywa hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara kushiriki. Wakati huo huo, Mhe. Shigella amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati ya kuwathamini wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa na kwamba matunda yatokanayo na madini yananufaisha watanzania. Amesema, miongoni mwa sheria zilizotungwa za asilimia 20 ya dhahabu kununuliwa na Benki Kuu, nia ni kuhakikisha Taifa linakua na akiba ya dhahabu ya kutosha. “Mwaka jana kilo moja ya dhahabu iliuzwa kwa Dola 50,000 kwa sasa kilo moja inakwenda kwa Dola 70,000,” amesema Mhe. Shigella na kuongeza ” Tungehifadhi dhahabu zetu tungekua na thamani kubwa kuliko kuhifadhi fedha za kigeni.” Amesisitiza Mhe. Shigella amewasihi wafanyabiashara waielewe Sheria hiyo, Benki Kuu imetoa taratibu za namna ya kununua dhahabu na kuondoa Tozo, bei iliyowekwa ni nzuri kuliko Dubai wanakopeleka.

RC SHIGELLA ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI Read More »

WIZARA YA MADINI, TUME YA MADINI NA BOT YAKUTANA NA WADAU WA MADINI

Ikiwa ni mkakati wa kutoa elimu kwa wadau wa madini kuhusu utekelezaji wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini Sura 123 WIZARA YA MADINI, TUME YA MADINI NA BOT YAKUTANA NA WADAU WA MADINI DODOMA Ikiwa ni mkakati wa kujenga uelewa kwa wadau wa madini kuhusu utekelezaji wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini Sura 123, leo Oktoba 04, 2024 Wizara ya Madini imeratibu mkutano wa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini uliofanyika jijini Dodoma ambapo elimu kuhusu utekelezaji wa sheria hiyo imetolewa na wataalam kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Viongozi walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Kamishna Msaidizi – Uendelezaji Migodi, Mhandisi Ally Samaje aliyemwakilisha Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, Meneja wa Masoko ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Lameck Kakulu, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, CPA. Venance Kasiki na watendaji wengine kutoka Tume ya Madini. Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga, Kamishna Msaidizi – Uendelezaji Migodi kutoka Wizara ya Madini, Mhandisi Ally Samaje amesema kuwa lengo la maboresho ya sheria hiyo inayomtaka kila mchimbaji na mfanyabiashara wa madini kutenga angalau asilimia 20 ya dhahabu inayozalishwa kwa ajili ya kuisafisha hapa nchini na kuiuzia BoT kabla ya kuisafirisha nje ya nchi ni kuimarisha uchumi wa nchi na kuongeza akiba (reserve) ya dhahabu nchini. Ameendelea kusema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wachimbaji na wafanyabiashara wa madini wanafanya kazi katika mazingira mazuri pasipo kuathiri biashara zao. Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo ameongeza kuwa sababu nyingine ya maboresho ya sheria hiyo ni kuhamasisha mnyororo wa shughuli za madini kufanyika nchini kuanzia kwenye uchimbaji, uchenjuaji, usafishaji na biashara ya madini. Wakati huohuo, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina sambamba na kuipongeza Serikali kwa maboresho ya Sheria za Madini ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kuendelea kuangalia namna bora ya kuwawezesha watanzania kushiriki katika Sekta ya Madini na kuendelea kutatua changamoto wanazokabiliana nazo wadau wa madini.

WIZARA YA MADINI, TUME YA MADINI NA BOT YAKUTANA NA WADAU WA MADINI Read More »

Scroll to Top